Loading...

Hizi hapa Takwimu za mechi zote za siku ya 'Boxing Day'.

BILA shaka siku ya ‘Boxing Day’ ilikuwa nzuri kwa mashabiki wa vigogo vya Premier League nchini England, kila mmoja alisherehekea ushindi kwa namna yake.

Hapa tumekuandalia takwimu mbalimbali zilizojitokeza katika michezo yote ya Premier League iliyochezwa siku ya Boxing day, karibu!

Hull City 0-3 Manchester City

Manchester City wameshinda michezo mitatu mfululizo kwa mara ya kwanza na kumaliza mkosi wao wa kupata matokeo mabaya ulioanza Septemba, mwaka huu.

Hull wameshinda mchezo mmoja tu katika michezo 16 ya EPL waliyocheza msimu huu, wamefungwa mara 12 na kupata sare tatu.

City walipata ‘clean sheet’ yao ya pili katika michezo 12 waliyocheza ugenini msimu huu.

Yaya Toure amefunga penalti zote 10 alizopiga kwenye Premier League na kuweka rekodi ya kipekee katika suala zima la kupiga mikwaju hiyo ya penalti.

Hull wamesababisha penalti tisa msimu huu na nane kati ya hizo wamefungwa.

Ni Jamie Vardy pekee aliyesababisha penalti nyingi (10) kwenye Premier League tangu msimu wa 2013/14, anayemfuatia ni Raheem Sterling aliyesababisha penalti 7.

Kwa mara 15, Hull City wametangulia kufungwa bao la kwanza kwenye michezo ya Premier League msimu huu, hakuna timu yenye rekodi hii zaidi yao.

Asisti 61 alizotoa David Silva zimemfanya kuwa kinara wa asisti nyingi kwenye Premier League tangu Agosti 2010 alipocheza mchezo wake wa kwanza nchini England.

Kelechi Iheanacho amefunga mabao 12 kwenye mashuti 19 yaliyolenga lango.

Watford 1-1 Crystal Palace


Kwa mara nyingine tena Sam Allardyce ameshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa kwanza akiwa na timu mpya, alishindwa kufanya hivyo pia alipokuwa na Sunderland.

Troy Deeney amekuwa mchezaji wa tano kwa Watford kufunga mabao 100 katika michuano yote aliyocheza baada ya Luther Blissett, Tommy Barnett, Ross Jenkins na Cliff Holton.

Deeney ndiye mfungaji bora wa Watford katika historia ya Premier League akiwa na mabao 17, nyuma yake anafuatiwa kwa karibu na Odion Ighalo mwenye mabao 16.

Christian Benteke ndiye mchezaji aliyekosa penalti nyingi zaidi msimu huu kwenye Premier League, amekosa penalti 2.

Crystal Palace wameruhusu nyavu zao kutikiswa katika michezo 22 kati ya 23 walioyocheza kwenye Premier League.

Yohan Cabaye amefanikiwa bao katika mechi zote alizocheza katika dimba la Vicarage Road.

Arsenal 1-0 West Bromwich Albion

Arsenal wamefanikiwa kufunga bao katika michezo yote 21 waliyocheza na Wesr Bromwich katika Premier League.

Tony Pulis amepoteza mechi zote tisa alizoiongoza timu yake kwenye Uwanja wa Emirates na kibaya zaidi, ana rekodi ya timu anayofundisha kufunga mabao matatu tu kwenye mechi zote tisa.

Mesut Ozil alicheza mchezo wake wa 100 kwenye Premier League na kutengeneza asisti yake ya 36, ni Eric Cantona pekee aliyetoa asisti nyingi (39) katika idadi hiyo ya mechi.

Olivier Giroud amefunga mabao saba kwenye mechi tano alizoanza kwenye kikosi cha kwanza msimu huu.

Kwa mara ya kwanza tangu Oktoba, Arsenal walicheza bila kuruhusu bao, huku West Brom kwa mara ya kwanza wakicheza mechi mbili mfululizo bila kufunga bao.

Burnley 1-0 Middlesbrough


Burnley walipata ushindi wao wa kwanza katika michezo saba waliyocheza dhidi ya Middlesbrough (wamepata sare 2 na kupoteza mara 4).

Katika michezo 22 ya Premier League Middlesbrough waliyocheza ugenini wamefanikiwa kushinda mara moja tu (sare 6 na kufungwa 15).

Burnley wamefanikiwa kufunga bao kwenye mechi nane kati ya tisa walizocheza katika uwanja wao wa Turf Moor.

Andre Gray amefunga bao la kwanza katika michezo 10 ya EPL aliyocheza msimu huu.

Pointi 19 kati ya 20 walizopata Burnley msimu huu wamezivuna wakiwa katika dimba lao la nyumbani.

Chelsea 3-0 Bournemouth

Kwa mara ya kwanza Chelsea wameshinda michezo 12 ya ligi mfululizo.

Antonio Conte ndiye kocha wa kwanza ndani ya Premier League kushinda mechi 15 kati ya 18 alizofundisha tangu aanze kazi.

Bournemouth wamepoteza mechi tatu kati ya nne za hivi karibuni na zote wamefungwa kuanzia mabao matatu.

Eden Hazard ni mchezaji wa sita katika kikosi cha Chelsea kufunga mabao 50 kwenye Premier League, watano waliotangulia ni Frank Lampard, Didier Drogba, Jimmy Floyd Hasselbaink, Gianfranco Zola na Eidur Gudjohnsen.

Cesc Fabregas ametengeneza asisti 98 tangu aingie kwenye Premier League. Ni Wayne Rooney (101), Frank Lampard (102) na Ryan Giggs (162) wenye asisti nyingi zaidi yake.

Fabregas amefunga na kuasisti katika michezo yote mitatu aliyoanza katika kikosi cha kwanza cha Chelsea (bao moja na asisti 2).

Leicester City 0-2 Everton


Leicester hawajawahi kushinda mchezo wa EPL siku ya Boxing Day tangu walivyomfunga Sheffield Wednesday bao 1-0 mwaka 1998 (sare 1 na kufungwa mara 6).

Ushindi wa bao 2-0 ugenini, uliwafanya Everton kumaliza mkosi wao wa kucheza michezo sita mfululizo bila ushindi.

Joel Robles amekuwa kipa wa 50 kupiga asisti katika histoaria ya Premier League nchini England.

Everton hawajapoteza mechi ya ugenini katika michezo mitano ya Premier League siku ya Boxing Day (ushindi 3 na sare 2).

Romelu Lukaku amefunga mabao saba kwenye michezo 11 ya Everton waliyocheza ugenini.

Kevin Mirallas amefanikiwa kufunga bao katika mechi tatu zote alizocheza na Leicester kwenye Premier League.

Everton wamepoteza mechi mbili tu kati ya 14 walizocheza na Leicester kwenye Premier League, wameshinda mechi 7 na kutoka sare 5.

Manchester United 3-1 Sunderland


Zlatan Ibrahimovic amehusika kwenye mabao 14 ya Manchester United mpaka sasa, akifunga 12 na kutengeneza mawili, idadi hii ni zaidi ya wachezaji wote wa United msimu huu.

Fabio Borini amefunga bao la kwanza tangu Mei alipofunga dhidi ya Chelsea.

Manchester United wameshinda mechi 19 za Premier League zilizochezwa siku ya Boxing Day, hakuna timu iliyoshinda michezo mingi zaidi yao.

Kwa mara ya kwanza Jose Mourinho amefanikiwa kushinda mechi 4 mfululizo tangu alivyofanya hivyo mara ya mwisho April 2015 akiwa na Chelsea.

Asisti zote tatu alizotoa Paul Pogba msimu huu ndani ya Premier League zimefungwa na Zlatan Ibrahimovic.

Baada ya kushindwa kufunga katika michezo 10 ya mwanzo akiwa na Manchester United, Henrikh Mkhitaryan alifanikiwa kufunga bao kwenye mchezo wa tatu mfululizo.

Sunderland wameshinda mchezo mmoja tu kati ya 25 waliyocheza ugenini dhidi ya Man United (sare 7 na kupoteza 17).

Swansea City 1-4 West Ham United


Kwa mara ya kwanza West Ham wameshinda mechi tatu mfululizo kwenye Premier League tangu Machi mwaka huu.

Swansea wamefungwa mabao 29 tangu Bob Bradley akabidhiwe kuinoa timu hiyo Oktoba 15 mwaka huu.

Mabao 9 kati ya 13 yaliyofungwa na Andre Ayew, ameyafunga katika Uwanja wa Liberty.

Ayew ni mchezaji wa 41 kufunga bao akiwa na West Ham na kuwafunga akiwa na jezi nyingine.

Swansea wameruhusu kufungwa bao la kwanza katika mechi 13 za Premier League walizocheza msimu huu, ni Hull City pekee waliofungwa mabao mengi zaidi yao.

Dimitri Payet ametoa asisti 15 kwenye Premier League kwa mwaka 2016, hakuna mchezaji mwenye asisti nyingi zaidi yake kwa mwaka huu.

Michail Antonio amefunga mabao 16 kwenye Premier League akiwa na jezi ya West Ham tangu msimu uliopita, hakuna mchezaji wa Wagonga nyundo aliyefunga zaidi yake.

Mabao yote aliyofunga Fernando Llorente msimu huu akiwa na jezi ya Swansea ameyafunga kwenye Uwanja wa Liberty.

Source: Dimba
ZeroDegree.
Hizi hapa Takwimu za mechi zote za siku ya 'Boxing Day'. Hizi hapa Takwimu za mechi zote za siku ya 'Boxing Day'. Reviewed by Zero Degree on 12/28/2016 11:45:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.