Loading...

Chanzo cha mgogoro kati ya Dangote na Serikali chabainishwa.

Wakati sakata la Dangote Indutries Tanzania kuhusu ukubwa wa gharama za uzalishaji likiendelea, Chama cha Wamiliki wa Malori (Tatoa) kimesema mpango wa malipo, bei waliyopewa na ubovu wa barabara vilikwamisha wanachama wake kukubaliana na kiwanda hicho cha kuzalisha saruji.

Wamiliki hao wa malori walitakiwa kuingia makubaliano na kiwanda hicho kwa ajili ya kukipelekea makaa ya mawe yanayochimbwa mkoani Songwe, zaidi ya kilomita 1,000 kutoka Mtwara, lakini hawakuweza kufanya hivyo.

“Hii biashara ya usafirishaji ni huria. Hakuna bei rasmi, ni makubaliano tu na sisi kama chama hatuwalazimishi wanachama wetu kuchukua mzigo wowote. Tulipofuatwa waliwaeleza wanachama wetu, wakaenda kukubaliana na Dangote,” alisema ofisa mtendaji mkuu wa Tatoa, Emmanuel Kakuyu.

Source: Mtembezi
ZeroDegree.
Chanzo cha mgogoro kati ya Dangote na Serikali chabainishwa. Chanzo cha mgogoro kati ya Dangote na Serikali chabainishwa. Reviewed by Zero Degree on 12/06/2016 12:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.