Loading...

FA imewashtaki Manchester city na Chelsea kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji.

Klabu za Manchester City na Chelsea zimeshtakiwa na FA kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji wakati wa mechi ya Ligi ya Premia iliyochezwa Jumamosi.

Mashtaka hayo yanatokana na mfarakano wa wachezaji uliozuka dakika ya 95 wakati wa mechi hiyo iliyochezewa Etihad ambapo Chelsea walishinda 3-1.

Mshambuliaji wa City Sergio Aguero na kiungo wa kati Fernandinho walifukuzwa uwanjani, lakini kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas hatachukuliwa hatua.


Wachezaji na maafisa wa klabu zote mbili walihusika katika mtafaruku huo.
Meneja wa City Pep Guardiola aliomba radhi kwa mchango wa timu yake katika kisa hicho.

Aguero, 28, amepigwa marufuku kucheza mechi nne kutokana na kisa chake hicho cha pili cha kufukuzwa uwanjani kwa utovu wa nidhamu, baada yake kumkabili visivyo beki wa Chelsea David Luiz.

Fernandinho walikabiliana na Fabregas baada ya kosa hilo la Aguero, na Mbrazil huyo atatumikia marufuku ya mechi tatu.

Klabu zote zimepewa hadi saa 18:00 GMT mnamo 8 Desemba kujibu mashtaka hayo.

ZeroDegree.
FA imewashtaki Manchester city na Chelsea kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji. FA imewashtaki Manchester city na Chelsea kwa kushindwa kuwadhibiti wachezaji. Reviewed by Zero Degree on 12/06/2016 11:54:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.