Ligi kuu ya England maarufu kama EPL huwa ina mabadiliko sana mchezaji anaweza akang’aa msimu mmoja msimu unaofuata akashindwa kutekeleza jukumu. Hii ndivyo ilivyo mifano mizuri Jamie Vardy, Ozil hata Hazard.
|
Jamie Vardy |
Msimu uliopita Ozil ndiye alikuwa kinara wa kutoa pasi za mwsho alipiga pasi 19 za magoli ambapo ilibaki moja afikishe rekodi ya Thiery Henry, japo haikuwa rahisi kwake kuzipata pasi zote hizo na huenda kama safu ya ushambuliaji ingetulia angeweza kuvuka rekodi ya Henry.
|
Mesut Ozil |
Hazard msimu uliopita hakuwa katika kiwango kizuri lakini msimu huu amerudi vyema sana, hivyo hivyo kwa Vardy alipata magoli 24 lakini msimu huu ametuama kama maji ya mtungi hii ndio maana halisi ya mchezo wa soka.
|
Eden Hazard |
Hadi sasa Kevin De Bruyne ndiye kinara wa pasi za mwisho ana nafasi za usaidizi 9 na magoli 6 ya kufunga hivyo wastani mkubwa sana kwake ikiwa bado miezi mitano ligi iishe. Huku nafasi ya pili ibashikwa na Alexis Sanchez akiwa amepata kusaidia nafasi 6 akiwa sambamba na Adam Lalalana. Idadi hii kabla ya mechi za ‘Boxing Day’.
|
Kevin De Bruyne |