Loading...

James kubaki Real Madrid, ..asema yuko tayari kupigania nafasi kikosi cha kwanza.

James Rodriguez amekuwa na wakati wa furaha na heka heka za hapa na pale tangu kuingia ligi ya La Liga, lakini kwa mujibu wa wakala wake, Nyota huyo toka Colombia yuko tayari kwa lolote kuendelea kubaki Hispania ili kupigania nafasi katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid.

Pamoja na kuhitajika kwa kiasi kikibwa na vilabu mbali mbali vya Ligi Kuu ya Uingereza, ikiwa ni pamoja na Chelsea na Manchester United, James anaweza kubaki na Klabu yake Real Madrid wakati wa usajili katika dilisha dogo mwezi Januari, kwa mujibu wa wakala wake Jorge Mendes.

"James hataondoka Real Madrid mwezi Januari," Mendes alisema hayo alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari nchini Spain.

Msimu huu, James amefunga mabao mawili tu katika michezo 16 ya mashindano yote aliyoshiriki.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 sasa ni msimu wake wa tatu katika klabu ya Madrid baada ya kujiungan na klabu hiyo akitokea Ligue 1 ya Ufaransa alipokuwa akiichezea klabu ya Monaco. Kimataifa, James amekuwa mtu muhimu katika mafanikio ya timu yake ya taifa ya Colombia tangu alipopata nafasi yake ya kwanza kuitumikia timu yake mwaka 2011.

ZeroDegree.
James kubaki Real Madrid, ..asema yuko tayari kupigania nafasi kikosi cha kwanza. James kubaki Real Madrid, ..asema yuko tayari kupigania nafasi kikosi cha kwanza. Reviewed by Zero Degree on 12/27/2016 05:56:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.