Loading...

Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino mbaroni kwa kuendesha gari akiwa amelewa.

Mchezaji wa klabu ya Liverpool Roberto Firmino ameshtakiwa kwa kosa la kuendesha gari akiwa mlevi baada ya kukamatwa mkesha wa siku ya Krismasi.

Mshambuliaji huyo ambaye ana umri wa miaka 25 alikamatwa baada ya gari lake kusimamishwa katikati mwa mji wa Liverpool mapema siku ya Jumamosi, polisi wamesema.

Firmino amabye ni raia wa Brazil anatarajiwa kufikishwa mbele ya hakimu wa Liverpool mnamo Januari 31. Atawasilishwa mahakamani siku ambayo timu yake itakuwa ikiikaribisha Chelsea katika uwanja wa Anfield.

Liverpool ilimsajili kutoka Hoffenheim kwa kandarasi ya miaka mitano iliogharimu kitita cha pauni milioni 29 mwezi Juni.

Liverpool imesema kuwa haitazungumzia swala hilo hadi pale hatua hiyo ya kisheria itakapokamilika.

ZeroDegree.
Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino mbaroni kwa kuendesha gari akiwa amelewa. Mshambuliaji wa Liverpool, Roberto Firmino mbaroni kwa kuendesha gari akiwa amelewa. Reviewed by Zero Degree on 12/27/2016 06:03:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.