Loading...

Ni vigumu kwa Man City kuikamata Chelsea kileleni, Pep Guardiola.

Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola anasema kuwa itakuwa vigumu kwa kikosi chake kushindana na viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea.

City ilipanda hadi nafasi ya pili katika jedwali baada ya kuicharaza Hull City 3-0 katika siku kuu ya Boxing Dei na kuweza kuwa nyuma ya Chelsea kwa pointi 7.

Kikosi hicho cha Antonio Conte awali kiliweka rekodi ya kushinda mara 12 katika ligi ya Uingereza baada ya kuichapa Bournemouth 3-0.

''Tumecheza mechi saba zaidi ya Chelsea ,ndio maana ni vigumu '',alisema Guradiola.

''Liverpool ilikaribia taji hilo mwaka mmoja uliopita kwa sababu walikuwa na mechi moja kwa wiki ,na ni hivyo ndivyo ilivyokuwa na Leicester.Mara hii Chelsea na Liverpool wana fursa''.

Liverpool na Chelsea zilishindwa kufuzu katika mashindano ya Ulaya baada ya kumaliza wa nane na 10 mtawalia katika ligi ya Uingereza mwaka uliopita.

ZeroDegree.
Ni vigumu kwa Man City kuikamata Chelsea kileleni, Pep Guardiola. Ni vigumu kwa Man City kuikamata Chelsea kileleni, Pep Guardiola. Reviewed by Zero Degree on 12/27/2016 06:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.