Loading...

Polisi 29 nchini Uturuki washtakiwa kwa lengo la kutaka kuipindua serikali.

Askari waliohusika katika jaribio la mapinduzi nchini Uturuki washtakiwa.
Takriban maafisa wa polisi 29 wanashtakiwa mjini Instabul Uturuki kwa kuhusika katika jaribio la mapinduzi mnamo mwezi Julai.

Kesi hiyo ndio muhimu zaidi kuwahi kufanyika huku zaidi ya mashtaka 1000 yakiandaliwa. Huku maafisa wengine 40 wakizuiliwa kesi hiyo inatarajiwa kuwa kubwa zaidi katika historia ya Uturuki ya leo.

Rais wa Uturuki katikati Reccep Tayip Erdogan.
Washukiwa wanashtakiwa kwa kuwa na lengo la kuipindua serikali mbali na kujihusisha na kundi linaloongozwa na muhubiri anayeishi Marekani Fethullah Gulen, ambaye mamlaka inamlaumu kwa kupanga njama hiyo.

ZeroDegree.
Polisi 29 nchini Uturuki washtakiwa kwa lengo la kutaka kuipindua serikali. Polisi 29 nchini Uturuki washtakiwa kwa lengo la kutaka kuipindua serikali. Reviewed by Zero Degree on 12/27/2016 02:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.