Loading...

Kaseja kupimwa tena leo wakati Kagera Sugar ikicheza dhidi ya Polisi Moro.

TIMU ya Kagera Sugar itashuka dimbani leo kuumana na Polisi Morogoro katika pambano la kujipima nguvu ambalo limepangwa kupigwa kwenye wa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Mchezo huo utakuwa wa pili kwa Kagera tangu ilipoingia kambini kujiandaa na duru la pili la Ligi Kuu Bara ambalo litaanza kurindima Desemba 17.

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Meck Mexime, alisema huo utakuwa mchezo wa mwisho kwao kabla ya kuelekea Mbeya ambako itafungua pazia la Ligi Kuu kwa kumenyana na Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine.

Alisema amekiandaa vizuri kwa ajili ya kuhakikisha kinafanya vizuri mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

“Mechi mbili za kirafiki zinanitosha, nimerekebisha kasoro zilizojitokeza mzunguko wa kwanza ikiwemo kusajili wachezaji wapya, ni matumaini yangu tutafanya vizuri mzunguko wa pili,” alisema Mexime.

Miongoni mwa wachezaji wapya wa Kagera Sugar waliosajiliwa kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo ni kipa mkongwe nchini, Juma Kaseja

Credits: Bingwa
ZeroDegree.
Kaseja kupimwa tena leo wakati Kagera Sugar ikicheza dhidi ya Polisi Moro. Kaseja kupimwa tena leo wakati Kagera Sugar ikicheza dhidi ya Polisi Moro. Reviewed by Zero Degree on 12/13/2016 01:26:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.