Kinachoendelea juu ya Tanzania na Nchi ya Malawi.
Serikali ya Tanzania imesema itafanya uchunguzi kuhusu habari zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Malawi vinavyodai majasusi wanane wa Tanzania wametiwa mbaroni wakifanya ujasusi katika mgodi mmoja wa urani katika nchi hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga ameliambia gazeti la The Citizen kuwa hana habari kuhusu ripoti hizo na kuahidi kufuatilia.
“Ndio kwanza nasikia habari hii kutoka kwako. Haya ni madai mazito. Nitafuatilia jioni hii. Nitawasiliana na ubalozi wetu Malawi na maafisa wetu wa intelijensia kujua zaidi kuhusu madai hayo. Haya ni madai mazito sana,” amesema Dk. Mahiga.
Vyombo vya habari vya Malawi vimezinukuu duru za usalama bila ya kutaja majina zikisema kuwa, baadhi ya Watanzania hao wamekamatwa na vifaa vinavyotia wasiwasi zikiwemo kamera zenye uwezo mkubwa wa kupiga picha.
Gazeti la kila siku la The Citizen la hapa nchini limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, taarifa za kutiwa mbaroni watu hao ziliripotiwa kwa mara ya kwanza siku ya Alhamisi na vyombo vya habari vya Malawi vikadai kuwa, majasusi wanane wametumwa na serikali ya Tanzania kwenda kuchunguza iwapo Malawi inaunda silaha za nyuklia kwa kutumia urani kwenye mgodi wa Kayerekera uliopo Wilayani Karonga ama la.
Waziri wa Mambo ya Nje na Masuala ya Afrika Mashariki, Dk. Augustine Mahiga ameliambia gazeti la The Citizen kuwa hana habari kuhusu ripoti hizo na kuahidi kufuatilia.
“Ndio kwanza nasikia habari hii kutoka kwako. Haya ni madai mazito. Nitafuatilia jioni hii. Nitawasiliana na ubalozi wetu Malawi na maafisa wetu wa intelijensia kujua zaidi kuhusu madai hayo. Haya ni madai mazito sana,” amesema Dk. Mahiga.
Vyombo vya habari vya Malawi vimezinukuu duru za usalama bila ya kutaja majina zikisema kuwa, baadhi ya Watanzania hao wamekamatwa na vifaa vinavyotia wasiwasi zikiwemo kamera zenye uwezo mkubwa wa kupiga picha.
ZeroDegree.
Kinachoendelea juu ya Tanzania na Nchi ya Malawi.
Reviewed by Zero Degree
on
12/27/2016 01:12:00 PM
Rating: