Loading...

Kipigo cha Cheka nchini India chazua utata.

Meneja wa bondia Francis Cheka, Juma Ndambile ameanza kuchunguza chanzo cha bondia huyo kupigwa kwa TKO na Vijender Singh wikiendi iliyopita huku akidai kipigo hicho kina utata.

Cheka alipigwa kwa TKO raundi ya tatu na Singh kwenye pambano la ubingwa wa mabara la WBO la uzani wa super middle kg 76 lililofanyika nchini India juzi usiku.

Pambano hilo lilimalizika ‘kiajabu’ baada ya mwamuzi kulimaliza wakati Cheka akiwa fiti amesimama kwenye kona akizungumza na kocha wake, Abdallah ‘Comando’ Salehe na msaidizi mwingine, Jay Msangi.

“Siyo kawaida ya Cheka kumaliza pambano hivyo, namjua nimefanya naye kazi, Cheka ni bondia mvumilivu, mwenyewe nilishangazwa na matokeo yale, sikujua nini kimetokea,” alisema Ndambile na kuongeza. “Kila Mtanzania anaweza kuwa shahidi katika hili, Cheka ni bondia mvumilivu, hadi apigwe kwa TKO au KO mpinzani wake amefanya kazi kwelikweli, lakini kwa Singh haikuwa hivyo, ndiyo sababu nasema kuna walakini.

“Tayari nimeanza kulifuatilia suala hili, kuna mtu ambaye yuko India, haifiki Ijumaa kila kitu juu ya pambano hilo kitajulikana,” alisema meneja wa Cheka, ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya ulinzi ya Advance Security.

Source: Nipashe
ZeroDegree.
Kipigo cha Cheka nchini India chazua utata.  Kipigo cha Cheka nchini India chazua utata. Reviewed by Zero Degree on 12/20/2016 05:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.