Loading...

Maalim Seif aibua upya sakata la mkono wa Rais Shein

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema kitendo chake cha kukataa kushikana mikono na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ni kuuthibitishia umma kwamba yeye si mnafiki.

Tukio hilo lilitokea Agosti, wakati wa maziko ya Rais wa Pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi yaliyofanyika makaburi ya Migombani ambako Maalim Seif alikataa kumpa mkono Dk Shein.

Hii ni mara ya kwanza kwa Maalim Seif kuzungumzia suala hilo.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi yaliyofanyika katika ofisi ya Makao Makuu ya CUF Mtendeni, Zanzibar juzi, Maalim Seif alisema Dk Shein anaujua ukweli kuhusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Mara kwa mara, Maalim Seif amekuwa akinukuliwa na vyombo vya habari akidai kwamba alishinda uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana kabla ya matokeo yake kufutwa na kurudiwa Machi 20, ambako yeye na chama chake walisusia.

ZeroDegree.
Maalim Seif aibua upya sakata la mkono wa Rais Shein Maalim Seif aibua upya sakata la mkono wa Rais Shein Reviewed by Zero Degree on 12/16/2016 10:17:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.