Maambukizi ya VVU nchini yashuka kwa asilimia 20.
- Chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI kufanyiwa majaribio Afrika Kusini.
- Mabadiliko yafanyika katika matumizi ya dawa za ARV.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk.Leonard Maboko wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika mkutano wa kujitambulisha kwao tangu ateuliwe na Rais Dk.John Magufuli kushika nafasi hiyo Julai 7 mwaka huu.
Amesema maambukizo mapya ya VVU yaliyokadiriwa kuwa watu milioni 2.1 kwa mwaka 2015 Duniani kote wakati maambukizo mapya yameshuka kwa asilimia 50 miongoni mwa watoto duniani.
Ameongeza kuwa watoto 290,000 wapya waliambukizwa mwaka 2010 na watoto 150,000 waliambukizwa mwaka 2015 ambapo maambukizo mapya kwa watu wazima hayajashuka tangu 2010 duniani.
Ameongeza kuwa watoto 290,000 wapya waliambukizwa mwaka 2010 na watoto 150,000 waliambukizwa mwaka 2015 ambapo maambukizo mapya kwa watu wazima hayajashuka tangu 2010 duniani.
Katika hatua nyingine Dk. Maboko alisema Tafiti zimeonesha kuwa wanawake ndio waathirika wakubwa wa maambukizo ya VVU kwa upande wa Tanzania Bara ukilinganisha na wanaume.
Amesema maambukizo VVU kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 wanawake wakionesha kuathirika zaidi kwa asilimia 6.2 ukilinganisha na wanaume ambao ni asilimia 3.8.
“Katika utafiti huo wa mwaka 2011 na 2012 ulionyesha kuwa Mkoa wa Njombe ulikuwa na kiwango kikubwa cha maambukizo ukiwa na asilimia 14.8 ukifuatiwa na Iringa kwa asilimia 9.1 na Mbeya kwa asilimia 9” alisema Dk.Maboko.
Dk.Maboko alisema Mkoa wa Manyara ulikuwa na kiwango kidogo cha maambukizo ya asilimia 1.5 lakini takwimu za ndani ya mkoa huo eneo la Mirelani kwenye mgodi wa Tanzanite maambukizo ya VVU yalikuwa ni asilimia 16 kiwango ambacho ni cha juu ya Mkoa wa Njombe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (Tacaids) Dk.Leonard Maboko (kushoto), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kulia ni Mkurugenzi wa Habari na Uraghibishi, Jumanne Issango. |
Dk. Maboko aliwaomba wananchi kote walipo kutobweteka kwa mafanikio yaliyo ya mapambano dhidhi ya VVU na ukimwi na kuwa yawe endelevu hata katika maeneo au mikoa ambako kuna maambukizo kidogo ya VVU.
Amesema kama nchi tunatakiwa kuweka nguvu nyingi kifedha na kimkakati katika maeneo na makundi yenye kiwango kikubwa cha maambukizo ya VVU ikiwa ni pamoja na kuimarisha utafiti na ukusanyaji wa takwimu za VVU na Ukimwi ili tuendelee kubaini na kupanga mipango dhidi ya ugonjwa huo inayoongozwa na takwimu.
Mkutano ukiendelea na wandishi wa habari. |
Dk. Maboko alitoa mwito kwa wananchi, Taasisi za kijamii, Serikali, watu binafsi na makampuni ya kibiashara kuchangia mfuko wa udhamini wa masuala ya ukimwi (AIDS TRUST FUND-ATF) ulioanzishwa na serikali ili kuondokana na utegemezi kwa wafadhili.
Wanahabari wakifuatilia kwa umakini. |
ZeroDegree.
Maambukizi ya VVU nchini yashuka kwa asilimia 20.
Reviewed by Zero Degree
on
12/29/2016 11:16:00 AM
Rating: