Loading...

Serikali imepiga marufuku matumizi ya vilainishi 'Grease/Oil' katika injini na mitambo.

Serikali imepiga marufuku vilainishi vyote vya injini na mitambo vya kupima baada ya kubaini kwamba vilainishi hivyo vimechakachuliwa na kupoteza ubora wake.

Uchunguzi uliofanywa na Ofisi ya Mkemia Mkuu umebaini kwamba zaidi ya asilimia 50 ya vilainishi vinavyouzwa sokoni havikidhi ubora wa viwango vya kitaifa.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamis Kigwangallah amesema serikali imefanikiwa kudhibiti uingizwaji wa vilainishi feki nchini lakini tatizo liko sokoni ambako baadhi ya wafanyabiashara wanachakachua na kuvipakia upya kwa nembo ya kampuni zinazoingiza vilainishi nchini.

Dk Kigwangallah amemwagiza Mkemia Mkuu kuendelea na uchunguzi na kuwabaini wanaouza vilainishi ambavyo havikidhi ubora kwa viwango vya kitaifa.

"Madhara ya kutumia vilainishi feki ni kuharibu injini za mitambo au magari. Pia, kunakuwa na tofauti ya bei katika soko kati ya bidhaa halisi na zile feki. Lakini kwa wafanyabiashara wanaouza vilainishi nje ya nchi wanaichafua Tanzania kwa kuuza bidhaa zisizokidhi vigezo,”amesema.

Amesema wizara yake imeanza kuandaa kanuni kwa ajili ya ufungishaji wa vilainishi na Mkemia Mkuu ataanza kutoa hati maalumu (certificate of analysis) kwa ajili ya kampuni zinazoingiza au kuuza nje vilainishi.

ZeroDegree.
Serikali imepiga marufuku matumizi ya vilainishi 'Grease/Oil' katika injini na mitambo. Serikali imepiga marufuku matumizi ya vilainishi 'Grease/Oil' katika injini na mitambo. Reviewed by Zero Degree on 12/20/2016 10:57:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.