Loading...

Haji Manara aiomba TFF imsamehe Jerry Muro.

MKUU wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Hajji Manara amemuomba Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi kumsamehe Mkuu wa Idara hiyo wa Yanga, Jerry Muro aliyefungiwa mwaka mmoja Julai mwaka huu.

Muro amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na masuala ya soka pamoja na kutozwa faini ya Sh. milioni tatu Julai mwaka huu baada ya Kamati ya Maadili ya TFF, chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Wilson Ogunde kumtia hatiani kwa mashtaka mawili kati ya matatu.

Makosa yaliyomtia hatiani Muro ni kudharau maamuzi ya Kamati ya Nidhamu ya TFF mwaka 2015 alipotakiwa kulipa faini ya Sh. milioni tano baada ya kufanya makosa, lakini akakaidi kulipa hadi leo.

Kwa kosa hilo alihukumiwa kutengana na masuala ya soka kwa mwaka mmoja- wakati shitaka lingine lililomtia hatiani ni kuchochea vurugu na kuhatarisha amani kuelekea mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na TP Mazembe ya DRC.

Katika shitaka hilo, Jerry anadaiwa kuwashawishi mashabiki wa Yanga kuwafanyia vurugu mashabiki wa Simba kwenye mchezo huo ambao timu yake ilifungwa 1-0 na Mazembe Juni 28, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Na akizungumza na Nipashe jana, Manara alimuomba Malinzi kumsamahe Muro baada ya kutumikia karibu nusu ya adhabu yake.

"Nimekaa nimetafakari sana, nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro, ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari amekwishatumikia karibia nusu ya kifungo chake,"alisema Manara.

"Nnajua kwa kufanya hivyo atakuwa amekwishajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa klabu kwa ujumla.

"Nafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi binafsi, lakini yale yalikwishapita na binafasi amenihakikishia hatorudia tena, na ninaamini viongozi na mashabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wana Simba," aliongeza Manara.

Aidha, Manara amemuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Muro, au kuziomba kamati zilizomfungia kumuachia huru, hususan ikizingatiwa si mzoefu sana wa utamaduni wa siasa za mchezo huu murua zaidi duniani.

ZeroDegree.
Haji Manara aiomba TFF imsamehe Jerry Muro. Haji Manara aiomba TFF imsamehe Jerry Muro. Reviewed by Zero Degree on 12/26/2016 02:42:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.