Loading...

Tanzania kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa [ UN ].

Wajumbe walioshiriki mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) anayeshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (wa pili kulia), ambapo masuala kadhaa yakiwemo maendeleo ya Sekta Binafsi na Miundombinu yalijadiliwa kwa kina wakati ujumbe huo kutoka UN ulipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Ofisini kwake Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) (wa kwanza kushoto), akielezea mpango wa Serikali wa kutumia malighafi za ndani katika kufikia maendeleo ya viwanda nchini, katika Kikao kati yake na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi Masikini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (wa kwanza kulia), Mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.
Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (kulia) akizungumza na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (hayupo pichani) kuhusu ushirikiano wa Tanzania na Umoja huo, Makao Makuu ya Wizara, Jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez.

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (kulia) na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez wakisikiliza kwa makini maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), (hayupo pichani), alipokuwa akielezea miradi itakayowakwamua wananchi kiuchumi ikiwemo ile ya Kilimo itakayosaidia kuendesha viwanda. Mazungumzo hayo yamefanyika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango, Jijini Dar es salaam.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa kwanza kushoto), akifurahia jambo wakati Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya (hayupo pichani), akielezea ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa, wakati wa kikao kilichofanyika Makao makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)

Wajumbe walioambatana na Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Maskini Duniani Bw. Gyan Chandra Acharya, wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb) alipokuwa akielezea umuhimu wa amani katika maendeleo ya Bara la Afrika, wakati wa kikao chake na Kiongozi huyo katika ukumbi wa Wizara ya Fedha na Mipango Jijini Dar es salaam.


ZeroDegree.
Tanzania kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa [ UN ]. Tanzania kuimarisha ushirikiano na Umoja wa Mataifa [ UN ]. Reviewed by Zero Degree on 12/07/2016 09:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.