Uhamiaji yawazuia wachezaji wa Kigeni Simba na Yanga.
SERIKALI kupitia Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, imezuia na kuwapiga marufuku wachezaji wote wa kigeni katika klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara kuzichezea timu hizo bila kupata kibali cha kufanya kazi nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishna wa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, John Msumule, alisema wamepokea taarifa zikiwahusisha wachezaji nyota wa klabu zote kubwa hapa nchini na wameonya juu ya klabu zao kuwatumia wachezaji hao.
Taarifa ambazo zimepatikana zinadai kuwa mbali na wachezaji wapya wa Simba waliodaiwa kukosa vibali vya kuwaruhusu kufanya kazi nchini, lakini pia wapo wachezaji wa zamani waliokuwepo kwenye timu tangu mwanzo wa msimu ambao walikatiwa vibali vya muda.
“Wachezaji kama Janvier Bokungu, Frederick Blagnon, Laudit Mavugo na Method Mwanjale wa Simba pamoja na makocha wao, Joseph Omog, Jackson Mayanja na kocha wa makipa, Abdul Idd Salim, hawa tumeelezwa kwamba walikatiwa vibali vya muda ambavyo vimeisha tayari hivyo tunaendelea kuangalia wengine,” alisema ofisa mmoja wa Uhamiaji ambaye hakutaka atajwe kwa kuwa yeye hana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo.
“Mimi nimeagizwa kuangalia mafaili yao, lakini taarifa rasmi atazitoa Kamishna, ila wengine hata hao wapya wameombewa ila nadhani kutokana na ile process ya kusema nani anasajiliwa nani anakatwa ndiyo maana vibali havikutoka kwa wakati,” alisema.
Alipotakiwa kuzungumzia taarifa hizo, Kamishna Msumule alisisitiza kwamba masuala haya ni ya sheria za nchi na anayevunja anachukuliwa hatua hivyo klabu itakayokiuka agizo hilo itachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kukiuka sheria za nchi.
“Sheria za nchi haziruhusu mtu yeyote kuishi au kufanya kazi kama hana kibali kinachomruhusu kufanya hivyo na yeyote atakayekwenda kinyume sheria itafuata mkondo wake, hivyo kwa tahadhari tu wasiwatumie wala kuwaruhusu kufanya nao kazi ikiwa hawajatimiza vigezo,” alisema Msumule.
Sakata hilo lilianza kutoka kwa Ndanda wakiilalamikia Simba kumchezesha kipa Agyei na kiungo Kotei bila kibali wakitaka kupewa pointi za chee jambo ambalo Serikali imeamua kulivalia njuga.
Msumule ametoa agizo hilo baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba Simba waliwachezesha Kotei na Agyei katika mchezo wao dhidi ya Ndanda uliopigwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Nangwanda bila vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.
Hata hivyo, imeelezwa kwamba Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina na kiungo, Justine Zulu, hawana vibali, ingawa kuna taarifa kuwa uongozi wa klabu hiyo ulifanya kazi yake ipasavyo.
Kwa upande wa Azam, Mtendaji wao Mkuu, Saadi Kawemba, alisema wachezaji na makocha wa timu hiyo wana vibali vya kufanya kazi na wala hawana wasiwasi wowote.
“Hakuna mchezaji wetu wala kocha ambaye anaishi kinyume cha sheria, sisi tulifanya kazi yetu vizuri ndiyo maana hatuna wasiwasi,” alisema.
Hata hivyo, juhudi kuwapata viongozi wa Simba na Yanga ziligonga mwamba, kwani simu za makatibu wao, Patrick Kahemele na Baraka Deusdedit ziliita bila kupokelewa.

Source: Bingwa
ZeroDegree.
Uhamiaji yawazuia wachezaji wa Kigeni Simba na Yanga.
Reviewed by Zero Degree
on
12/22/2016 11:44:00 AM
Rating: