Loading...

VIDEO: Jinsi Man City ilivyoaibika kwenye uwanja wa nyumbani.

Chelsea imefanikiwa kushinda kikwazo kikubwa kama ilivooneka kwa vijana wa Antonio Conte ulivokuwa ukipigana baada ya kuwa nyuma ya maadui zao kwa goli 1-0 kwa kuwapiga watu tisa wa Manchester City 3-1 kwenye Uwanja wao wa Etihad siku ya leo Jumamosi na kufikisha mechi nane za ushindi mfululizo katika ligi kuu ya uingereza.


Bao la kujifunga kutoka kwa Gary Cahill karibia na mapumziko liliwafanya Man City kuongoza mechi kwa kipindi kifupi, lakini mabao mawili ndani ya dakika 10 kutoka Diego Costa na Willian yakageuza mchezo juu ya kichwa. Man City walipoteza nafasi nyingi wakati Chelsea ilionyesha kuwa kamili, mbali na hayo mawili, Eden Hazard akaongeza goli jingine la tatu katika dakika za majeruhi, huku Sergio Aguero na Fernandinho wakitolewa wote kwa kadi nyekundu katika dakika za majeruhi baada ya kuonekana kuwa na jazba.

Sambamba na ushindi huo, Chelsea bado iko juu ya msimamo wa ligi kuu ikiwa na pointi 34, wakati City ikibaki na pointi 30 baada ya mateso makubwa ya kupoteza mechi ya pili ya msimu.

Man City walionekana kuwa kelele nyingi za kugombea adhabu ya penati wakati David Silva alipojaribu kuupitisha mpira umzunguke ya Cahill na mpira ukagonga mkono wa beki huyo wa Chelsea, lakini mwamuzi Anthony Taylor akatupilia mbali madai hayo.

Ndipo Chelsea ikaenda karibu na ushinfi wakati Hazard alipopiga shuti fupi la kimo cha chini ambapo ilipatikana na kadi ya njano ya kwanza ya mchezo aliyoonyeshwa Nicolas Otamendi baada y akumchezea rafu.

Aguero alikaribia kupata ushindi katika na fasi mbili alizopata na kuonyesha juhudi kubwa ya kutaka kupata goli lakini juhudi zote zikatibuliwa na Thibaut Courtois alionekana pia na juhudi zaidi kulinda mlango wake.

Mchezo uliamsha kelele za mashabiki pale Fernandinho alipokuwa akimalizia 'free kick' ya Kevin De Bruyne lakini bendera ya kuotea ikapandishwa juu na mwamuzi wa pembeni. Muda mfupi baadaye Hazard alipata nafasi ya wazi na badala yake alijaribu 
alitoa kwa mwenzie lakini Man city walikuwa tayari wameimarisha ulinzi vizuri na hatimaye chelsea kupoteza nafasi hiyo.

Wakati utata ulipoonekana baada Aguero 
kugongana na David Luiz ambaye alikuwa beki wa mwisho katika safu ya ulinzi lakini Taylor hakutoa adhabu yoyote. Aguero alikaribia ushindi na Cesar Azpilicueta akamtibulia mipango wakati huo city ilikuwa mbele kwa goli moja kabla ya mapumziko.

Dakika za mwanzo za nusu ya pili Man City alikuwa na nafasi nzuri ya kuongeza bao la pili wakati Leroy Sane alipoanzisha mpira na kuutuma kwa De Bruyne lakini shuti lake halikuwa na madhara kwa Courtois. Wakati upande mwingine Costa naye alikimbiza mpira hadi ufanikiwa kuingia ndani ya sanduku lakini shuti lake alilopiga likaenda nje ya goli.

Katika dakika ya 60 Chelsea walipata nafasi iliyotengenezwa na Cesc Fabreags (ambaye unaweza sema yumo kikosini kwa sababu tu Nemanja Matic ni malijeruhi) alituma mpira mrefu ambapo Costa aliutulizia kifuani na kuutia nyavuni na kufanya matokeo kuwa ni 1-1.

Costa alitulia vema hakika na kucheza kwa tukufu, kwa mara nyingine tena, na kumpa nafasi Willian ambaye alichimbua kombora la chini na kuyaweka matoke yakiwa na chelsea akiongoza kwa goli 2-1.




Chelsea iliendelea kucheza na makali katika safu ya ulinzi. Hata hivyo, vijana wa Antonio Conte waliongeza raha zaidi kwa kushinda bao jingine tena ambapo Marcos Alonso alituma mpira mrefukwa Hazard ambaye alitumia nafasi yake ya wazi na kumaliza ubishi kwa kuutupi nyavuni na kufanya matokeo kuwa 3-1.

Katika dakika za majeruhi Aguero alionyeshwa kadi nyekundu kumchezea rafu Davis Luiz na baadaye ikatokea rafu nyingine tena aliyochezewa Fabregas kwa kusukumwa ndani na Fernandinho ambaye pia alitolewa nje kwa kadi nyekundu na kuwafanya City wamalize mchezo na-watu tisa pekee.

Ukiachana na habari zote hizo, hii ilikuwa ni nusu ya pili ya ajabu kutokea kwa Chelsea ambayo imewapa heshima na kuwafanya waendele kubakia juu katika msima wa ligi, na kumwacha Guardiola na wachezaji wake na ngumu ya kufanya kuitafuta nafasi ya kwanza.



ZeroDegree.
VIDEO: Jinsi Man City ilivyoaibika kwenye uwanja wa nyumbani. VIDEO: Jinsi Man City ilivyoaibika kwenye uwanja wa nyumbani. Reviewed by Zero Degree on 12/03/2016 10:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.