Loading...

Wafahamu nini maana ya 2G, 3G, 4G na 5G? Soma ufafanuzi hapa.

Katika sekta ya mawasiliano, ni kawaida kuwasikia wataalamu na wakati mwingine watu wa kawaida wakizungumzia kuhusu teknolojia ya 2G, 3G, 4G na 5G. Maana yake ni nini?

G kwenye tarakimu hizi inawakilisha 'Generation', yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa data kwenye simu.

Hakuna kipimo chochote kinachotumiwa kimataifa kuhusu kasi ya data ya simu.

Lakini wengi wanakubaliana kuhusu baadhi ya sifa za teknolojia hizi.

Teknolojia ya 1G, au kizazi cha kwanza cha data ya simu, ilianza kutumiwa 1991.

Teknolojia ya 2G ilianza pia kutumika katika kipindi hicho, ikiwa kama ndugu wa 1G.

Kwa 1G, ungeweza tu kupiga simu

Teknolojia hii sana ilikuwa analogu na simu za wakati huo zilikuwa kama hizi hapa chini...



Kisha 2G ikaja na uwezo wa kutuma ujumbe mfupi au arafa

Teknolojia ya 2G ambayo pia huitwa teknolojia ya SMS iliwezesha watu kutuma ujumbe mfupi.

Ungeweza pia kutuma ujumbe wenye picha, ambao uliitwa MMS (multimedia messaging service).

Na pia simu za wakati huo zilikuwa na teknolojia ya GSM, GPRS, EDGE kama hizi zilizo hapa chini.



Kupiga simu kwa video kuliwezekana 2001
3G na kasi yake ya data ya 2mbit/s (megabaiti 0.25 kila sekunde) ilianza kutumika wakati ambao simu za kwanza aina ya smartphone zilianza kuuzwa madukani.

Huduma yake ya mtandao haikuwa ya kasi sana lakini iliwezesha huduma ya mtandao kupatikana bila kutumia nyaya. Angalau ilikuwa hatua fulani kubwa, na watu waliweza kupiga simu za video.

Ili kufahamu kasi yake au mwendo wake wa upole ulivyokuwa, iwapo ungetaka kupakua filamu ya ucheshi ya David Brent: Life on the Road kutoka kwenye iTunes, ingekuchukua saa tano kupakua faili hiyo ya 4.26GB.

2010 teknolojia ya 4G ikaanza kutumika

Teknolojia hii ya kasi iliwezesha kuanza kupatikana kwa michezo mingi kwenye simu na ya kiwango cha juu.

Filamu ambayo ingekuchukua saa tano kuipakua kwa teknolojia ya 3G sasa inaweza ikakuchukua dakika 8 pekee kwa teknolojia ya 4G.

Lakini 4G haipatikani maeneo yote, hata katika mataifa yaliyoendelea.

Afrika Mashariki, utaipata katika baadhi ya maeneo ya miji mikubwa.

5G ndiyo mwendo kasi?

Hii ndiyo ya kasi zaidi kwa sasa.

Tume ya Mawasiliano ya Ulaya inakadiria kwamba kati ya mwaka 2020 na 2030, utaweza kupakua filamu moja ya HD ya saa moja kwa sekunde sita pekee.

Simu za wakati huo nazo zitakuwa na muonekano gani? Kama hii hapa chini labda?


Source: BBC Swahili
ZeroDegree.
Wafahamu nini maana ya 2G, 3G, 4G na 5G? Soma ufafanuzi hapa. Wafahamu nini maana ya 2G, 3G, 4G na 5G? Soma ufafanuzi hapa. Reviewed by Zero Degree on 12/21/2016 12:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.