Kampuni ya Simu Tanzania [TTCL] kuanza kutoa huduma za kifedha mwakani.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameitaka Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) kujipanga na kuanza mkakati wa kutangaza huduma za fedha ambazo zitatolewa na kampuni hiyo mwanzoni mwa mwaka ujao.
Prof. Mbarawa ametoa agizo hilo baada ya kukagua mitambo itakayotumika kwa huduma hiyo ambayo itaongeza ushindani wa biashara kwenye huduma za simu nchini mkoani Dodoma.
“Lazima mjipange kwenye idara ya masoko kwa kuanza kutangaza huduma hiyo kupitia njia zote zikiwemo mitandao ya kijamii, ili wananchi warahisishiwe huduma za fedha kupitia TTCL”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha, ameiagiza kampuni hiyo kupitia idara ya masoko kujipanga kuona fursa zilizopo kwa kufahamu mahitaji ya wateja wao na kuhakikisha inaongeza wateja katika mkoa huo ili kuteka soko la ushindani ambapo Serikali inajipanga kuhamia huko.

Waziri Prof.Mbarawa ametaja baadhi ya maeneo ambayo TTCL inahitaji kuboresha zaidi ni upande wa Simu (Voice) na Data (video) ili kuweza kurahisisha mawasiliano kwa njia ya video conference kwa kuwa kuna baadhi ya watendaji wengine watabaki Dar es salaam.
“Mkiimarisha mawasiliano upande wa data mtarahisisha hata maamuzi na pia kazi zitaenda vizuri Serikalini hasa ukizingatia baadhi ya watumishi watakuwa hapa Dodoma na wengine Dar es Salaam”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Sambamba na hilo, Waziri Mbarawa ameliagiza Shirika la Posta nchini kuja na mkakati wa kuandaa matangazo ya kutambulisha huduma ya Posta mlangoni kwa jamii ili kuiwezesha huduma hiyo kutambulika kirahisi.

Amesisitiza kwa Taasisi hizo kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ili kufikia malengo waliojiwekea na kuendana na kasi ya utendaji wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Akiwa mkoani humo Prof. Mbarawa amemhakikishia Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana kuboresha miundombinu nchini hususan katika mkoa huo ikiwemo kuboresha usafiri wa anga katika uwanja wa ndege wa Dodoma ili kuruhusu ndege kubwa kuweza kuruka na kutua.
Katika hatua nyingine, Waziri Mbarawa ameongea na watendaji pamoja na wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara yake na kusisitiza kufanya kazi kwa kasi, uadilifu, ubunifu na kushirikiana katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku.

Akizungumza kwa niaba ya wafanyakazi hao Meneja wa Wakala wa Majengo(TBA) mkoani humo, Arch. Masalu Bururu, amemuahidi Waziri huyo kutekeleza yale yote aliyowà agiza ili kuleta ufanisi na tija kwa Taifa.
Waziri Prof. Mbarawa amemaliza ziara yake ya siku kumi katika mikoa ya Mwanza, Mara, Arusha, Manyara na Dodoma ambapo ametembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Wizara hiyo.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa, akizungumza na watumishi wa taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo (hawapo pichani), alipokutana nao Mkoani Dodoma. |
ZeroDegree.
Kampuni ya Simu Tanzania [TTCL] kuanza kutoa huduma za kifedha mwakani.
Reviewed by Zero Degree
on
12/21/2016 11:34:00 AM
Rating: