Loading...

Wastani wa wanafunzi 6 wilayani Same hupata mimba katika kila mwezi.

WANAFUNZI 63 wa shule mbalimbali za sekondari Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wamepata mimba katika kipindi cha Januari hadi Oktoba, mwaka huu.

Ofisa Elimu Sekondari wilayani humo, Happiness Laiser, aliyasema hayo juzi katika Kikao cha Baraza la Madiwani.
“Hali hii imetokana na umbali wanaotembea wanafunzi wengi hasa wa kike, kukutana na vishawishi vingi njiani,” alisema.

Alisema ili kukabiliana na changamoto hiyo, uongozi wa halmashauri hiyo umeanza mikakati mbalimbali ukiwemo wa kuhamasisha ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa kike wilayani humo.

“Pia tumeanza mikakati ya kuelimisha jamii umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike, kutoa ushauri nasaha katika shule zote za sekondari na elimu ya afya ya uzazi,” alisema.

Aliongeza kuwa, uongozi wa halmashauri hiyo ukishirikiana na uongozi wa kata, vijiji, vitongoji na wakuu wa shule, wameanza mikakati ya kuwabaini wanaume waliowapa mimba wanafunzi ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.

ZeroDegree.
Wastani wa wanafunzi 6 wilayani Same hupata mimba katika kila mwezi. Wastani wa wanafunzi 6 wilayani Same hupata mimba katika kila mwezi. Reviewed by Zero Degree on 12/13/2016 12:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.