Loading...

6 wauwa kwa kupigwa risasi wakiwa Msikitini

Watu sita wanaripotiwa kupoteza maisha na wengine nane wakiwa majeruhi baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana baada ya kuwavamia wakati wakiwa msikitini jijini Quebec, Canada.

Polisi Quebec wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa limetokea usiku wa Jumapili wakati watu hao wakiwa msikitini ambapo tukio lilitokea wakiwa wamemaliza kusali.

Msemaji wa Polisi amesema tayari wanawashikilia watu wawili kwa kudaiwa kuhusika na tukio hilo ambapo mmoja wao alikamatwa karibu na eneo ambalo shambulizi hilo lilifanyika na mwingine akikamatwa maili 14 kutoka eneo la tukio na alikuwa akiondoka kwenda sehemu nyingine.

“Tukio limedhibitiwa, majengo ni salama na wakazi walihamishwa,” ilisema sehemu ya taaifa na kuongeza, “Upelelezi unaendelea.”

Aidha inaripotiwa kuwa wakati watu hao wanavamia msikitini kufanya shambulio hilo kulikuwa na watu wanaokadiriwa kuwa kati ya 60 hadi 100 na Serikali ya Canada imesema tukio hilo lina viashiria kuwa ni la kigaidi.
6 wauwa kwa kupigwa risasi wakiwa Msikitini 6 wauwa kwa kupigwa risasi wakiwa Msikitini Reviewed by Zero Degree on 1/30/2017 12:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.