Loading...

Golikipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom afariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili

Golikipa wa timu ya Kagera Sugar, David Abdalah Burhan ambaye pia amewahi kuchezea klabu mbalimbali za ligi kuu amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando.

Kipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2013/2014, David Abdallah Burhan amefariki dunia asubuhi ya leo katika hospitali ya Bugando, Mwanza.

Kipa huyo wa Kagera Sugar ya Bukoba alifikishwa hospitalini hapo jana kutoka Bukoba na kwa bahati mbaya asubuhi ya leo ameaga dunia.

Kocha wa Kagera Sugar, Mecky Mexime Kianga amesema kwamba Burhan, mtoto huyo wa mshambuliaji wa zamani wa Pan Africans, Abdallah Burhan alikuwa anasumbuliwa na Malaria.

Mexime alisema matatizo hayo yalianza wakati wamekwenda Singida kucheza na wenyeji, Singida United mechi ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Kombe la Azam Sports Federation (ASFC) katikati ya wiki.


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amethibitisha kutokea kifi hicho na kutuma salamu zake za pole kwa familia pamoja na klabu ya Kagera Sugar na kwa wote ambao wameguswa na kifo cha mchezaji huyo.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha David Abdalah Burhan mchezaji wa Kagera Sugar. Amefariki usiku wa kuamkia leo.Apumzike kwa amani,” alitweet kiongozi huyo wa TFF.

Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kurejeshwa kwao Iringa na kuhusu mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Kagera Sugar na Mtibwa Sugar Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Mexime amesema kwamba hawajajua kama utachezwa au la.

“Sasa hivi ndiyo tunakwenda kwenye kikao cha kabla ya mechi, tukifika huko ndiyo tutajua, ila kwa kweli upande wetu wachezaji wote wameshitushwa mno na taarifa hizi na sidhani kama wapo tayari kwa mechi ya leo,”alisema.

Marehemu David Burhan ameshawahidakia Mbeya City na Majimaji, ikumbukwe kuwa Burhan ni mtoto wa mshambuliaji wa zamani wa Pan African ya Dar es Salaam, Abdallah Buruhan.

ZeroDegree.
Golikipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom afariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili Golikipa bora wa Ligi Kuu ya Vodacom afariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili Reviewed by Zero Degree on 1/30/2017 12:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.