Loading...

Baada ya kipigo toka kwa Prisons, ..Mbeya City yatupa lawama zote kwa mabeki

MBEYA City imewatupia lawama mabeki wake baada ya kipigo cha jana cha mabao 2-0 kutoka kwa mahasimu wao wa Jiji la Mbeya, Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini humo.

Akizungumza baada ya mchezo huo, ambao mabao ya Mohammed Samatta na Benjamin Asukile yaliwaliza majogoo hao wa jiji la Mbeya, Kocha Msaidizi , Mohammed Kijuso, alisema kwamba makosa ya mabeki yaliwapa nafasi Prisons kufunga mabao mawili jana.

“Ni makosa kadhaa yaliyofanywa na safu yetu ya ulinzi leo (Jana) yamesababisha kupoteza mchezo huu wa Ligi Kuu dhidi ya Prison kwa mabao 2-0, tumeuzunishwa na matokeo haya lakini lazima tuyakubali”alisema Kijuso, mshambuliaji wa zamani wa Simba.

Pamoja na hayo, Kijuso alisema hayo matokeo hayo ni sehemu ya mchezo na sasa wanasahau matokeo hayo na kuangalia michezo inayofuata.

Kijuso pia alisikitikia nafasi ambazo timu yake ilitengeneza katika mchezo huo, lakini ikashindwa kuzitumi ingawa alisisitiza kusema yote hayo ni mambo ya soka.

“Zimekuwa dakika 90 zenye makosa kadhaa, hili limetugharimu, tulitengeneza nafasi tukashindwa kuzitumia, baada ya makosa kadhaa wenzetu walipata nafasi mbili wakazitumia, hakuna namna nyingine tumekubalina na matokeo na tunarudi kwenda kurekebisha makosa yetu kabla ya mchezo wetu ujao,”alisema.

Kipigo cha jana kinaifanya Mbeya City ibaki nafasi ya nane kwa pointi zake 25 baada ya kucheza mechi 20, wakati Prisons inatoka nafasi ya 11 hadi ya nafasi ya sita ikifikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 21. Mbeya City, inayonolewa na na Mmalawi Kinnah Phiri, itashuka tena dimbani Februari 4 kumenyana na JKT Ruvu Uwanja wa Sokoine, siku ambayo Prisons watakuwa wageni wa Mwadui.

ZeroDegree.
Baada ya kipigo toka kwa Prisons, ..Mbeya City yatupa lawama zote kwa mabeki Baada ya kipigo toka kwa Prisons, ..Mbeya City yatupa lawama zote kwa mabeki Reviewed by Zero Degree on 1/30/2017 12:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.