Afcon: Ivory Coast watupwa nje na Morocco, DRC nao wafuzu hatua ya robo fainali
Bingwa mtetezi wa michuano ya kombe la mataifa ya afrika tembo wa Africa Ivory Coast, wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu baada ya kuchapwa kwa bao 1-0 na Simba wa Atlas Morocco.
Mabao ya DRC jana yalifungwa na Junior Kabananga dakika ya 29, Firmino Mubele dakika ya 54 na Paul-Jose 'M'Poku dakika ya 80, wakati la Togo lilifungwa na Kodjo Fo-Doh Laba dakika ya 69.
Hatua ya makundi itahitimishwa leo kwa mechi za Kundi D kati ya Uganda na Mali Uwanja wa d'Oyem na Misri na Ghana Uwanja wa Port Gentil, mechi zote zikianza Saa 4:00.
Ghana inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Misri yenye pointi nne, Mali pointi moja na Uganda haina pointi.
Goli pekee liliowaondoa miamba hao wa soka wa Afrika mashindanoni lilifungwa na Rachid Alioui katika dakika ya 64 ya mchezo.
Nayo timu ya Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo ilitambia Togo kwa kuichapa kwa mabao 3-1 na hivyo kufuzu hatua ya robo fainali wakiwa vinara kwa kundi C kwa alama 7 huku Moroco wakiwa nafasi ya pili kwa alama 6.
Moroco na Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo wanafuzu katika kundi hilo la huku Ivory Coast na Togo zikitupwa nje ya michuano hiyo.
Wachezaji wa Moroco wakishangilia |
Moroco na Jamuhuri ya kidemocrasia ya Congo wanafuzu katika kundi hilo la huku Ivory Coast na Togo zikitupwa nje ya michuano hiyo.
Hatua ya makundi itahitimishwa leo kwa mechi za Kundi D kati ya Uganda na Mali Uwanja wa d'Oyem na Misri na Ghana Uwanja wa Port Gentil, mechi zote zikianza Saa 4:00.
Ghana inaongoza Kundi hilo kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na Misri yenye pointi nne, Mali pointi moja na Uganda haina pointi.
ZeroDegree.
Afcon: Ivory Coast watupwa nje na Morocco, DRC nao wafuzu hatua ya robo fainali
Reviewed by Zero Degree
on
1/25/2017 11:00:00 AM
Rating: