Loading...

Chelsea yaifikia rekodi ya Arsenal ya ushindi.

Chelsea imeshinda mechi yake ya 13 mfululizo katika mchuano wa ligi kuu ya Uingereza Premier League.

Sasa inawiana na rekodi kama hiyo ya Arsenal.

Wakiongozwa na meneja wao Antonio Conte Chelsea imeishinda Stoke City mabao manne kwa mawili huko Stamford Bridge.

Kwa hivyo ni sherehe mara mbili - mwaka mpya na pointi sita mbele ya nambari mbili ambao ni Liverpool, walioicharaza Manchester City bao 
moja bila la kufunga mwaka 2016.

Hatahivyo, Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte amesema kuwa lengo la Chelsea sio rekodi bali ni taji la Uingereza.

ZeroDegree.
Chelsea yaifikia rekodi ya Arsenal ya ushindi. Chelsea yaifikia rekodi ya Arsenal ya ushindi. Reviewed by Zero Degree on 1/01/2017 05:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.