Gazeti la MwanaHalisi lapewa masaa 24 kumuomba radhi Rais Magufuli
Gazeti la MwanaHALISI limepewa saa 24 kumwomba radhi Rais John Magufuli kutokana na kuchapisha habari yenye kichwa, ““Ufisadi ndani ya ofisi ya JPM.”
Taarifa ya Idara ya Habari-Maelezo iliyotolewa leo imesema habari hiyo iliyochapishwa katika toleo la Jumatatu, Januari 30-Februari 5, 2017, inajenga dhana kuwa Rais Magufuli anahusika na kilichoitwa ufisadi wakati msingi wa taarifa husika ni tatizo la manunuzi katika Shirika la Elimu Kibaha!
“Kwa kuwa ni jambo lililodhahiri kuwa Shirika la Elimu Kibaha si ofisi, idara wala kitengo “ndani ya ofisi ya JPM” mwandishi na mhariri wa habari husika wamedhihirisha malengo ya kumchafua Rais binafsi kwa jamii.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi awa Maelezo, Hassan Abbas, ilisema katika siku za karibuni Serikali imejitahidi kufanya mazungumzo na wahariri wa gazeti hilo kwa lengo la kukumbushana maadili ya uandishi wa habari, lakini “bahati mbaya kwamba wamekuwa wakikaidi japo wito tu”.
“Kwa sababu hizi, Serikali inawaagiza wahariri wa gazeti hilo kujitathmini na kuchukua hatua kwa kutumia kifungu cha 40 cha Sheria ya Huduma za Habari, 2016 kinachowapa fursa ya kuomba radhi, kwa kumuomba radhi Rais ndani ya saa 24 kuanzia saa 10 jioni ya leo Januari 30, 2017.” Ilisema kuwa iwapo wahusika wataona muhali kufanya hivyo, Serikali itachukua hatua kali kwa mujibu wa sheria na masharti ya usajili ya gazeti husika.

Reviewed by Zero Degree
on
1/30/2017 11:15:00 PM
Rating: