Majambazi yateka kijiji na kupora milioni 13 wilayani Kilindi.
Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi waliokuwa na silaha za moto na baridi wameteka kijiji cha Kileguru kilichopo kata ya Kwediboma wilayani Kilindi kwa kutumia risasi kisha kumpora mfanyabiashara Anold Kiwelu fedha na mali zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 13.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa saba na nusu usiku limesababisha baadhi ya watu watatu Hamis Juma Maguno,David Tulo, Samwel na Asha Iddy Lungo waliotoka nje kwa ajili ya kwenda kusaidia kupigwa risasi na kujeruhiwa vibaya ambapo hivi sasa wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya matibabu.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Kwediboma Mwajuma Semphule akielezea tukio hilo,ameliomba jeshi la polisi kuongeza askari katika kituo cha polisi kilichojengwa na wananchi kisha kuwapa silaha za moto kwa sababu hili ni tukio la sita kutokea katika kipindi cha miezi mitano lakini kulingana na umbali uliopo wa kilomita 60 kutoka makao makuu ya wilaya ya Kilindi hadi eneo la tukio ni mbali ni vyema askari wakapewa silaha ili kudhibiti tatizo hilo.
Kufuatia hatua hiyo kamanda wa polisi mkoani Tanga Benedict Wakulyamba amesema hivi sasa jeshi lake lipo katika eneo la tukio kwa ajili ya kuwasaka wahalifu na amewataka wananchi kutoa ushirikiano bila kuogopa vitisho kwa sababu jeshi litaongeza ulinzi ili kuwadhibiti majambazi hayo.
Source: ITV
Majambazi yateka kijiji na kupora milioni 13 wilayani Kilindi.
Reviewed by Zero Degree
on
1/30/2017 11:40:00 PM
Rating: