Loading...

Guardiola akiri kushindwa na soka la Uingereza.

Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola amefunguka kuhusu soka la Uingereza kufuatia siku za karibuni kuonekana kushindwa kwenda na kasi ambayo alianza nayo wakati amejiunga Manchester City baada ya kuondoka Bayern Munich ya Ujerumani.

Guardiola alisema mwanzoni mwa msimu timu yake ilianza vizuri lakini baadae mambo yalikuwa tofauti kutokana na aina ya soka la Uingereza linavyochezwa hivyo anatamani soka la Uingereza limbadilishe ili aweze kwenda nalo sawa.



“Mwanzoni mwa msimu tulikuwa na matokeo mazuri na tulicheza vizuri, lakini baada ya kuwa na udhaifu katika eneo la ulinzi wakati wa mchezo wa Tottenham na Celtic hatukujiamini tena na kuanza kucheza kidogo na hata kwa wakati huo mawazo yangu hayakuwa sawa,

“Sababu nilikuwa bado nataka kuwajua wachezaji, sehemu gani nzuri wanacheza, namna nzuri ya kucheza na kuwazoea. Muda mwingine niliwaza kupanga wachezaji watatu na muda mwingine hilo halifanyi kazi na hilo likitokea linakuwa linamhusu meneja na siwezi kuwalaumu wachezaji sababu naona hilo tangu wakiwa katika mazoezi,” alisema Guardiola na kuongeza.

“Sikuja Uingereza kwa ajili ya kubadilisha aina ya uchezaji, sihitaji kufanya hivyo, nimekuja ili inibadilishe na ndiyo sababu ya mimi kuja hapa ili nibadilishwe, ni jambo zuri na kila nchi ina aina yake ya soka, aina yake ya uchezaji na hilo ndilo jambo la kushangaza.”

ZeroDegree.
Guardiola akiri kushindwa na soka la Uingereza. Guardiola akiri kushindwa na soka la Uingereza. Reviewed by Zero Degree on 1/08/2017 04:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.