Mtibwa Sugar yaanzisha tuzo zake.
Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser. |
Mratibu wa Mtibwa Sugar, Jamal Bayser aliiambia Nipashe jana kwamba zoezi hilo litaanza rasmi mwishoni mwa msimu kwa kuwashirikisha mashabiki wa timu hiyo.
Bayser alisema kwamba jopo la wataalamu litasimamia mchakato huo kuhakikisha wanapatikana wachezaji bora wanaostahili baada ya kura za mashabiki wa Mtibwa.
“Lengo kuu la utoaji wa tuzo hizi ni kuwapongeza na kuwapa hamasa na morali ya kufanya vizuri zaidi wachezaji ambao wanajitolea kwa ajili ya timu, lakini pia kujenga ushindani na kutoa msukumo kwa wachezaji wengine kupambana kwa ajili ya timu,”alisema Bayser na kuongeza.
“Lakini pia kuonyesha nidhamu ya juu na ushirikiano mzuri kwa timu, benchi la ufundi na viongozi.
Wachezaji watakaofanikiwa kupata tuzo hizi watakuwa ni wale watakaopigiwa kura nyingi zaidi na mashabiki wa Mtibwa Sugar.”
Alisema kuna mchakato maalum ambao mashabiki wa Mtibwa Sugar watajulishwa kupitia makundi yao mbalimbali ya mitandao ya kijamii juu ya namna ya upigaji kura.

ZeroDegree.
Mtibwa Sugar yaanzisha tuzo zake.
Reviewed by Zero Degree
on
1/08/2017 12:43:00 PM
Rating: