Hatimaye Emmanuel Adebayor apata timu mpya baada ya kukaa miezi 6 kama mchezaji huru
Emmanuel Adebayor amesaini mkataba na klabu inayoshiriki ligi kuu ya nchini Uturuki, stanbul Başakşehir. klabu hiyo ni ya pili katika Ligi Kuu ya Uturuki, nyuma ya mahasimu wao Besiktas.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu za Arsenal, Man City na Tottenham amekuwa mchezaji huru kwa muda wa miezi sita tangu kuondoka Crystal Palace msimu uliopita.
Kwa mujibu wa 'BeINSPORTS' ya Uturuki , Adebayor amesaini mkataba wa miezi 18 na klabu hiyo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 aliweza kufunga bao moja tu akiwa na klabu ya Crystal Palace msimu uliopita baada ya kukaa miezi sita akiwa 'Selhurst Park'.
Adebayor alikuwa akihusishwa na kujiunga na klabu ya mabingwa Besiktas, lakini baadhi ya ripoti zimeeleza kuwa klabu hiyo haikuwa tayari kukidhi mahitaji nyota huyo.
Yeye alikuwa anahitaji kulipwa mshahara wa kiasi cha £3million kwa mwaka (karibu sawa na £58,000 kwa wiki) lakini Beskitas - ambao kwa sasa wako juu kwenye msimamo wa Ligi kuu ya Uturuki - walikuwa tayari kumlipa £2m kwa mwaka.
Na hapo ndipo klabu ya Başakşehir ilipotia mguu ndani ya mazungumzo na nyota huyo.
klabu ya Istanbul ilimaliza katika nafasi ya nne katika msimu wa Ligi kuu mwaka jana, na ndio ilikuwa nafasi yao bora kumaliza katika mara zote ambazo imeshiriki mashindano hayo.
Mshambuliaji huyo wa Togo alijumuishwa pia kwenye kikosi cha Taifa lake katika Kombe la Mataifa ya Afrika, lakini walishindwa kufuzu mtoano katika hatua ya makundi, na kumaliza nafasi ya mwisho katika Kundi C.

Reviewed by Zero Degree
on
1/31/2017 06:57:00 PM
Rating: