Loading...

Hii ndio Timu pekee ya Zanzibar iliyofanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali Mapinduzi Cup

Taifa Jang’ombe ndio timu pekee kutoka Zanzibar ambayo imefuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la Mapinduzi kwa mwaka 2017.

Taifa imefuzu baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya URA ya Uganda ambao ndio walikuwa mabingwa watetezi wa taji hilo. Bao la Mohamed Said ‘Messi wa Unguja’ limeifanya Taifa ifikishe pointi tisa pointi moja nyuma ya Simba ambao ni vinara wa Kundi A.

Taifa Jang’ombe imefuzu ikizipiku timu nyingine za Zanzibar kama KVZ na mahasimu wao Jang’ombe Boys.



Watacheza nusu fainali ya kwanza saa 10:15 jioni Jumanne January 10 dhidi ya Azam ambao ndio vinara wa Kundi A.

Taifa Jang’ombe imeungana na iimu nyingine zilizofuzu hatua ya nusu fainali ni pamoja na Azam, Yanga na Simba ambazo zote zinatoka Tanzania bara.

ZeroDegree.
Hii ndio Timu pekee ya Zanzibar iliyofanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali Mapinduzi Cup Hii ndio Timu pekee ya Zanzibar iliyofanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali Mapinduzi Cup Reviewed by Zero Degree on 1/09/2017 12:41:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.