Jeshi la polisi lafanikiwa kuua majambazi watatu jijini Dar
Mmoja wa majambazi aliyeuwawa wakati wa tukio la ujambazi Mikocheni, Dar es Salaam |
- Polisi Dar yataja matukio makubwa ya mwaka 2016.
- Watuhumiwa wa ujambazi na madawa ya kulevya zaidi 13,000 wamekamatwa jijini Dar
- Wachina mbaroni jijini dar kwa utekaji.
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi, wameuawa katika tukio la kurushiana risasi na polisi katika eneo la Mikocheni, karibu na Shule ya Sekondari Feza jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro watuhumiwa hao waliuawa jana asubuhi na majina yao bado hayajafahamika.
Alisema marehemu hao ni waliohusika katika tukio la kupora zaidi ya Sh milioni 26 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro |
Alisema kwamba miili ya marehemu, imehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Baadhi ya mitandao ya kijamii, jana ilidai kwamba watuhumiwa hao akiwemo mwanamke aliyejisalimisha, ambaye ndiye alikuwa dereva wao, walikuwa na mpango wa kufanya uvamizi katika maeneo hayo, ambapo pia baadhi yao walifanikiwa kukimbia.
Wengine walidai walitaka kuvamia ofisi za Bima zilizpo karibu na eneo hilo. Lakini, Polisi haikuthibitisha taarifa hizo na kueleza wataeleza zaidi leo. Gazeti hili juzi asubuhi lilishuhudia tukio la uporaji Tazara, ambalo watuhumiwa wanadaiwa kuhusika, wakati gari hilo likiwa kwenye foleni ya magari.
Watu hao waliporwa katika eneo hilo ambalo askari doria huwa wametanda, lakini wakikamata pikipiki zinazotokea eneo la Buguruni.
Majambazi hao waliokuwa watatu, wanadaiwa kupora fedha hizo katika gari ndogo aina ya Toyota Rav 4 yenye namba za usajili T 455 DFN, mali ya kampuni ya kutengeneza mabati ya Sun Share, iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina la Richard Charles.
Kwenye gari pia alikuwepo mfanyakazi mwingine wa kampuni hiyo, mwenye asili ya China, aliyetambulika kwa jina la Cheng Deng na kwamba fedha hizo zilikuwa zikipelekwa benki.
Charles alisema majambazi hao, walimwamrisha kufungua mlango na kuwapatia begi la fedha, lililokuwa limewekwa katika kiti cha nyuma huku wakimtishia kwa bastola, kabla ya kuvunja kioo cha nyuma cha gari hilo na kubeba fedha hizo na kutokomea nazo.
ZeroDegree.
Jeshi la polisi lafanikiwa kuua majambazi watatu jijini Dar
Reviewed by Zero Degree
on
1/05/2017 09:25:00 AM
Rating: