Loading...

John Obi Mikel aihama rasmi klabu ya Chelsea na kutimkia China.

Kiungo wa kati wa Nigeria John Obi Mikel amekuwa mchezaji wa karibuni zaidi kuondoka Chelsea na kuhamia Ligi Kuu ya China.

Mikel ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba atajiunga na klabu ya Tianjin TEDA. Majuzi, Oscar aliondoka Stamford Bridge na kujiunga na Shanghai SIPG. Ikumbukwe kuwa mchezaji wa Brazil Ramires aliaagana klabu hiyo mwaka jana.

Mikel, ambaye amekaa miaka 10 Chelsea, hajapata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza msimu huu chini ya meneja wa sasa Antonio Conte.


Mikel ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na Europa League akiwa na Chelsea.

Amesema kwenye taarifa: "Kama mnavyofahamu, sijacheza sana msimu huu kama ambavyo ningelipenda, na ikizingatiwa kwamba nina miaka 29, nina miaka mingi sana ya kucheza."



Taarifa za habari zinasema amehama kutoka London bila kulipiwa pesa zozote na atakuwa akilipwa takriban pauni 140,000 ($173,432) kila wiki.


ZeroDegree.
John Obi Mikel aihama rasmi klabu ya Chelsea na kutimkia China. John Obi Mikel aihama rasmi klabu ya Chelsea na kutimkia China. Reviewed by Zero Degree on 1/06/2017 12:33:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.