Loading...

Mambo 10 usiyoyajua kuhusu msanii Drake.

WENGI wanamfahamu kwa jina la Drake, lakini jina alilopewa na wazazi wake ni Aubrey Drake Graham. Huyo ni miongoni mwa wasanii wa muziki wenye jina kubwa nchini Marekani na ulimwenguni kote.

Kwa sasa jina lake limekuwa sehemu ya vyombo vya habari kutokana na uhusiano wake wa kimapenzi na mwanamama Jenifer Lopez ‘J-Lo’.

Wapo wanaoamini kuwa Drake ameamua kutoka na J-Lo ili kumuumiza P. Diddy ambaye pia aliwahi kuwa mpenzi wa mwanamama huyo. Tuachane na hayo.
Bila shaka kuna mengi usiyoyajua kuhusu Drake na makala haya yanakuletea mambo 10 ambayo huenda hukuyafahamu kuhusu rapa huyo mwenye umri wa miaka 31.

  1. Drake ni miongoni mwa wasanii waliothibitisha kuwa hakuna kinachoshindikana hapa duniani. Wakati ananza muziki, alitaka kuwa na utajiri wa dola za Marekani milioni 25. Hivi sasa ana utajiri wa mola milioni 250. Weka malengo yako kwani hakuna kinachoshindikana chini ya jua.
  2. Oktoba mwaka jana Drake alivunja rekodi ya kuwa msanii aliyewania tuzo nyingi za muziki za Marekani. Alikuwa akipigania vipengele 13. Kabla yake, ni Michael Jackson ambaye alikuwa amewania vipengele 11. Lakini, licha ya kuwania vipengele 13, Drake alishinda tuzo moja pekee.
  3. Umaarufu wake ulianzia kwenye tamthilia ya Degrassi: The Next Generation, ambayo ilikuwa ikirushwa na kituo kimoja cha televisheni cha nchini Canada. Kipindi hicho Drake alikuwa na umri wa miaka 15 na alikuwa akiigiza kama mchezji wa mpira wa kikapu aliyevunjika mguu baada ya kupigwa risasi.
  4. Mbali na Jenifer Lopez aliyenaye hivi sasa, Drake aliwahi kutoka kimapenzi na mwanadada mwenye vituko vingi, Rihanna. Warembo wengine ambao Drake aliwahi kutoka nao ni staa wa tenesi, Serena Williams na Tyra Banks.
  5. Drake si mwanamuziki wa kwanza kwenye familia yao. Baba yake mzazi, Dennis Graham, alikuwa miongoni wa wanamuziki wa mkongwe Jerry Lee Lewis. Lakini pia, mjomba wake, Larry Graham, alikuwa mpiga gitaa wa Prince.
  6. Mbali na suti yake nzuri anaposhika ‘mic’, pia Drake ni mkali wa kuandika. Amewahi kuwa mwandishi wa nyimbo za akina Alicia Keys na Jamie Foxx. Kama ulikuwa hujui, “Un-Thinkable” ya Alicia Keys iliandikwa na mshikaji huyo pamoja na ile ya “Fall For Your Type” ya Jamie Foxx.
  7. Drake ni miongoni mwa mastaa wanaopenda sana mpira wa kikapu na timu anayoishabikia ni Miami Heat inayoshiriki NBA.
  8. Baada ya kusota sana kimaisha, nyumba yake ya kwanza baada ya kuwa tajiri ilimgharimu kiasi cha Dola za Marekani milioni 7 (zaid ya shilingi bilioni 14 za Kitanzania) na iko jijini Los Angeles.
  9. Niwambie tu kuwa Drake huwa hatumii daftari kuandika mistari. Mara nyingi simu yake ndiyo hutumika pale anapotaka kuandika.
  10. Drake ni mmoja kati ya wasanii wakorofi nchini Marekani. Amewahi kuhusishwa kwenye bifu na mastaa wenzake kama Tory Lanez, DMX, Ludacris, Kendrick Lamar, Jay Z, Common na Pusha T.
ZeroDegree.
Mambo 10 usiyoyajua kuhusu msanii Drake. Mambo 10 usiyoyajua kuhusu msanii Drake. Reviewed by Zero Degree on 1/06/2017 01:30:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.