Loading...

Kisa AFCON 2017, ..Adebayor aitolea nje klabu ya Olympique Lyon

Mchezaji wa zamani wa Arsenal, Emmanuel Adebayor amesema kabla ya kuanza kwa mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika ambayo kwa mwaka huu yanafanyika nchini Gabon, klabu ya Lyon ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Ufaransa ilitaka kumsajili lakini hakuwa tayari.

Adebayor amesema ilikuwa ni muhimu kwake kuliwakilisha taifa lake katika mashindano hayo makubwa barani Afrika na hata sasa kama ikitokea timu kubwa ikihitaji kumsajili hayupo tayari kujiunga hadi mashindano yamalizike.

“Nilikataa ofa ya makataba kutoka kwa Lyon kwa ajili tu nije kuiwakilisha nchi yangu, waliniuliza kama nitakuja katika ANC [Kombe la Mataifa Afrika] nikawambia ndiyo,

“Lazima niende kwa ajili ya kuisaidia nchi yangu, hakuna sababu ya kuacha kwenda ANC, hata kama ni timu bora duniani ikiniambia njoo kesho, sitakwenda,” alisema Adebayor.

ZeroDegree.
Kisa AFCON 2017, ..Adebayor aitolea nje klabu ya Olympique Lyon Kisa AFCON 2017, ..Adebayor aitolea nje klabu ya Olympique Lyon Reviewed by Zero Degree on 1/19/2017 07:59:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.