Loading...

Waziri Nape kufanya oparesheni ya kudhibiti wauza CD feki

Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni , Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema anatarajia kufanya oparesheni ya kukagua wenye mitambo ya kuzalisha CD feki na wauzaji wa kazi za wasanii bila kibali ambayo ni endelevu.

Waziri Nape amesema kwa muda mrefu sasa wasanii wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kutengeneza filamu lakini kuna baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekuwa wakitengeneza faida kubwa kutokana na kuuza nakala feki za kazi hizo.

Pamoja na hilo, pia aliwataka wasanii na wadau wa sanaa kutoa ushirikiano wa kutoka katika oparesheni hizo ili kuhakikisha tatizo hilo linapungua kama si kuisha kabisa nchini na kila mmoja akapata faida kutokana na kazi yake.

Amesistiza kuwa sekta ya filamu kwa sasa inakubwa na changamoto kubwa kutokana na kutokuwapo kwa Sera, kanuni na sheria na kuwa Sera ya filamu ambayo ipo kwenye maandalizi ikikamilika hayo yote yatakuwa historia.

Hata hivyo, aliwataka wasanii kuachana na unafiki, majungu na fitina ili wafanye kazi kwa kushirikiana katika kuielimisha jamii pamoja na kuchangia pato la Taifa kupitia kazi zao.

ZeroDegree.
Waziri Nape kufanya oparesheni ya kudhibiti wauza CD feki Waziri Nape kufanya oparesheni ya kudhibiti wauza CD feki Reviewed by Zero Degree on 1/19/2017 08:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.