Loading...

Msimamo wa Tanzania juu ya mpaka katika Ziwa Nyasa

Mindi Kasiga. 
WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, imesema Tanzania bado imeshikilia msimamo wake wa mpaka katika Ziwa Nyasa kuwa upo katikati ya ziwa licha ya Malawi kueleza upo ufukweni.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka wizara hiyo, Mindi Kasiga, aliliambia Nipashe kuwa licha ya mgogoro huo mpaka sasa kuwa mikononi mwa wasuluhishi, lakini Tanzana bado ina msimamo wake ikiamini kuwa mpaka wa ziwa hilo upo katikati na siyo katika fukwe kama nchi ya Malawi wanavyoeleza.

“Jopo la marais wastaafu likiongozwa na Rais wa zamani wa Msumbiji, Joachim Chissano, wanaendelea na usuluhishi, sisi Tanzania bado tuna msimamo kuwa mpaka upite katikati ya ziwa, lakini Malawi wao wanataka mpaka upite katika fukwe,” alisema Kasiga.

Alisema awali jopo hilo liliwahi kuwaita wabunge wa nchi za Malawi na Tanzania wenye majimbo yaliyopakana na ziwa hilo na kuwaeleza kuhusu mpaka wa ziwa hilo bila ya kuathiri mazigira ya nchi zote mbili.

Source: Nipashe
ZeroDegree.
Msimamo wa Tanzania juu ya mpaka katika Ziwa Nyasa Msimamo wa Tanzania juu ya mpaka katika Ziwa Nyasa Reviewed by Zero Degree on 1/06/2017 10:33:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.