Loading...

TANZIA: Mwanamke wa kwanza kugombea Urais nchini, Dk Anna Senkoro afariki dunia.

Marehemu Anna Senkoro (Aliyekaa katikati) 
Huenda jopo la madaktari bingwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) wangeokoa maisha ya mgombea wa kwanza wa Urais mwanamke, Dk Anna Senkoro iwapo angekubali kulazwa kwa ajili ya matibabu katika kitengo hicho juzi (Jumanne) usiku.

Mwanamke wa kwanza kwenye historia ya Tanzania kugombea urais kupitia Chama cha PPT Maendeleo, Dk Anna Claudia Senkoro amefariki dunia.

Senkoro aliyeamsha hamasa ya wanawake kuwania nafasi za juu za uongozi hapa nchini, alifariki dunia jana asubuhi nyumbani kwake Tabata Segerea jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Aminiel Eligaishi alithibitisha hospitali hiyo kupokea mwili wa mwanasiasa huyo na kubainisha kuwa umehifadhiwa katika chumba cha maiti hospitalini hapo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizolifikia gazeti hili, mauti yalimkuta Senkoro baada ya kuugua ghafla usiku wa kuamkia jana na kufariki majira ya asubuhi.

Senkoro aligombea nafasi ya urais wa Tanzania kupitia Chama cha PPT-Maendeleo mwaka 2005, akichuana na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete aliyegombea kwa tiketi wa CCM. Kikwete alishinda uchaguzi huo kwa kupata kura milioni 9. 12 sawa na asilimia 80.28.

Katika uchaguzi huo, wagombea wengine wa urais waliochuana na mwanamama huyo ni Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF aliyepata kura milioni 1.3 sawa na asilimia 11.68, Freeman Mbowe wa Chadema aliyepata kura 668.756 sawa na asilimia 5.8 na Augustine Mrema wa TLP aliyepata kura 84,901 sawa na 0.75.

Wengine ni Dk Sengondo Mvungi (NCCR-Mageuzi) aliyepata kura 55,819 sawa na asilimia 0.49, Mchungaji Christopher Mtikila (DP) aliyepata kura 31,083 sawa na asilimia 0.27, Dk Emmanuel Makaidi (NLD) aliyepata kura 21,574 sawa na asilimia 0.19.

Mvungi, Mtikila na Makaidi wamefariki dunia. Senkoro alipata kura 18,783 sawa na asilimia 0.17. Pamoja hao wengine ni Leonard Shayo (MAKINI) aliyepata kura 17,070 sawa na asilimia 0.15, Paul Kyara (SAU) aliyepata kura 16,414 sawa na asilimia 0.14.

Senkoro pamoja na kuwania nafasi ya urais akiwa PPTMaendeleo, chama ambacho tayari kimefutwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, mauti hayo yamekuta akiwa mwanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), ambako alihamia mwaka jana kutokana na vuguvugu la uchaguzi.

ZeroDegree.
TANZIA: Mwanamke wa kwanza kugombea Urais nchini, Dk Anna Senkoro afariki dunia. TANZIA: Mwanamke wa kwanza kugombea Urais nchini, Dk Anna Senkoro afariki dunia. Reviewed by Zero Degree on 1/05/2017 09:14:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.