Loading...

Waziri Nape amteua mkurugenzi mpya wa Idara ya Maendeleo ya Michezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemteua Yusuph Omari kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo kujaza nafasi iliyo achwa wazi na Leornad Thadeo aliyehamishiwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Kabla ya uteuzi huo, Omari alikuwa mkufunzi mwandamizi katika Chuo Kikuu cha Ardhi katika masuala ya michezo.

Nnauye pia limshukuru aliyekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda wote, Alex Nkenyenge ambaye alifanya kazi zake kwa uadilifu na kujituma kwa kusimamia majukumu yote ya idara kwa ukamilifu.

Aidha, ametoa wito kwa wanamichezo na wananchi kwa ujumla kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Omari atakapokuwa anatekeleza majukumu yake.


Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo, Yusuph Omari.


ZeroDegree.
Waziri Nape amteua mkurugenzi mpya wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Waziri Nape amteua mkurugenzi mpya wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Reviewed by Zero Degree on 1/11/2017 08:36:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.