Yanga gonjwa lilelile
YANGA imeendelea kukumbwa na ugonjwa wa kupiga penalti ambapo ndani ya kipindi cha miezi 16 imepoteza mashindano manne tofauti kwa tatizo la upigaji mbovu wa mikwaju ya penalti.
Juzi Jumanne usiku Yanga ilipoteza mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba kwa mikwaju 4-2 ya penalti ambapo kipa Deo Munishi ‘Dida’ na beki Mwinyi Haji walikosa mikwaju hiyo.
Mapema wakati msimu wa Ligi Kuu Bara unaanza, Yanga ilipoteza mchezo wa Ngao ya Hisani kwa Azam kwa mikwaju hiyo hiyo ya penalti. Mchezo huo wa Ngao ya Hisani ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2 katika dakika 90.
Katika mchezo huo nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima na Hassan Kessy walikosa mikwaju ya penalti ambayo ilipelekea timu hiyo kupoteza taji.
Mwaka jana Yanga iliondoshwa tena katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa mikwaju ya penalti dhidi ya URA ya Uganda ambayo ilikwenda kutwaa taji hilo. Nyota wa Yanga, Geofrey Mwashiuya na Malimi Busungu walikosa mikwaju ya penalti.
Rekodi hiyo mbaya ilianza pia katika michuano ya Kombe la Kagame Julai 2015, Yanga ilipoteza mchezo wa robo fainali kwa Azam kwa mikwaju hiyo hiyo ya penalti baada ya sare tasa katika dakika 90.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa ushindani mkubwa zaidi katika michuano hiyo ya Afrika Mashariki na Kati, nyota wa Yanga Mwinyi Haji alikosa penalti ambayo ilihitimisha safari ya Yanga.
Hii inamaanisha kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu uliopita Yanga imeshinda mchezo mmoja tu kwa mikwaju ya penalti ambapo ilikuwa mchezo wa Ngao ya Hisani dhidi ya Azam mwezi Agosti 2015.

Source: Mwanaspoti
ZeroDegree.
Yanga gonjwa lilelile
Reviewed by Zero Degree
on
1/13/2017 12:34:00 PM
Rating: