Loading...

Afcon: Camerron yaiong'oa Ghana kutoka mashindanoni kwa ushindi wa goli 2 bila [Video]

Cameroon watakutana na Misri katika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika 2017 baada ya magoli mawili ya kipindi cha pili kuiondosha Ghana katika mashindano hayo.

Timu zote mbili zilicheza mchezo wa kuvutia huku ikishuhudiwa kipindi cha kwanza zikimaliza kwa sare ya bila kufungana.

Wachezaji wa Cameroon wakipongezana baada ya kumalizika kwa mchezo kati yao na Ghana
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo milango ya kila timu iliendelea kuwa migumu mpaka dakika ya 72 Michael Ngadeu-Ngadjui alipofunga goli la kwanza kwa Cameroon.

Zikiwa zimesalia sekunde chache huku Ghana wakijaribu kusawazisha, Christian Bassogog alifunga goli la pili na kuzamisha kabisa matumaini ya Ghana kwa mwaka huu.

Matumanini ya Ghana kuchukua kikombe hicho ambacho kwa mara ya mwisho walikibeba mwaka 1982 sasa yamefikia mwisho katika michuano ya mwaka huu.

Mara ya mwisho kwa Cameroon kuingia fainali ilikuwa mwaka 2008 walipofungwa na Misri ambao ndio wanakutana nao tena katika fainali ya mwaka huu.


Afcon: Camerron yaiong'oa Ghana kutoka mashindanoni kwa ushindi wa goli 2 bila [Video] Afcon: Camerron yaiong'oa Ghana kutoka mashindanoni kwa ushindi wa goli 2 bila [Video] Reviewed by Zero Degree on 2/03/2017 11:59:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.