Loading...

Wanachama waja juu baada ya Jerry Muro kutemwa Yanga

BAADA ya uongozi wa Yanga kuamua kupitisha panga kwa baadhi ya wafanyakazi wake, akiwemo mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano cha klabu hiyo, Jerry Muro, kumeibuka gumzo juu ya suala hilo.

Baadhi ya wanachama wa Yanga, wamekuja juu na kuutaka uongozi wa klabu hiyo kubatilisha maamuzi yake ya kumfungashia virago Murokwani alikuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya klabu hiyo.

Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo ile inayomilikiwa na klabu hiyo, wanachama hao wamedai kuwa kama ni uongozi huo umechukua uamuzi huo wa kufungashia virago Muro kwa sababu ya ukata ni mara kumi akapunguzwa mtu mwingine lakini siyo Muro.

Baadhi ya baadhi wanachama jana walikusanyika makao makuu ya klabu hiyo kwa lengo la kutaka kuonana na uongozi wa klabu hiyo ili usitishe zoezi hilo la kufungashia virago Muro lakini hakufanikiwa kuonana na uongozi huo.

Hata hivyo alipoulizwa Muro kama tayari ameshakabidhiwa barua ya kufungashiwa virago na uongozi wa Yanga alisema: “Sijapata barua yoyote na wala sina taarifa hizo.”

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, amedai kusikitishwa na uamuzi huo uliofikiwa na uongozi dhidi ya Muro na amedai: “Sina mengi ya kusema ila Muro anatakiwa kujua kuwa kiongozi wetu huyo hivyo ndivyo alivyo ila mchango wake ndani ya Yanga nitaendelea kuutambua.”
Wanachama waja juu baada ya Jerry Muro kutemwa Yanga Wanachama waja juu baada ya Jerry Muro kutemwa Yanga Reviewed by Zero Degree on 2/03/2017 11:51:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.