Aliyeiongoza Hong Kong kati ya 2005-2012, Donald Tsang ahukumiwa kwenda jela kwa tuhuma za rushwa
![]() |
Donald Tsang (katikati) akiwa kwenye gari la wafungwa akisafirishwa kupelekwa Gerezani kutokea mahamani baada ya hukumu |
Tsang aliongoza Hong Kong kati ya 2005 na 2012 na ndiye afisa wa ngazi ya juu zaidi nchini humo kuwahi kushtakiwa kutokana na tuhuma za ulaji rushwa.
![]() |
Waandishi wa habari wakilizunguka gari la kubebea wafungwa gari ambalo alipandishwa Donald Tsang kutokea mahakamani |
![]() |
Tsang akiwasili kortini wakati wa kutolewa kwa hukumu |
Viongozi kadha wakuu wa zamani Hong Kong walikuwa wameandika barua kwa mahakama kumtetea Tsang.
Tsang aliondolewa makosa wiki iliyopita kuhusu shtaka la pili la kutumia vibaya mamlaka.
![]() |
Donald Tsang na mkewe Selina |
Baada ya kuhukumiwa, Tsang alitolewa kortini akiwa amefungwa pingu na kupelekwa hadi hospitalini ambapo amekuwa tangu Jumatatu baada ya kupatwa na maumivu ya kifua.
Aliyeiongoza Hong Kong kati ya 2005-2012, Donald Tsang ahukumiwa kwenda jela kwa tuhuma za rushwa
Reviewed by Zero Degree
on
2/22/2017 01:02:00 PM
Rating:
