Loading...

Askofu Gwajima aahidi kutoa ushirikiano Polisi

ASKOFU wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, amesema ameitikia wito uliotolewa na Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ya kumtaka kuripoti katika kituo hicho saa tatu asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kituo Kikuu cha Polisi jana, alisema kwa sababu ni wito halali uliotolewa na polisi, hivyo basi ataendelea kushirikiana na jeshi hilo ili kuhakikisha kuwa suala hilo linakwisha.

“Nilikuwa miongoni mwa washukiwa wa dawa za kulevya, lakini walinipima na ‘kusachi’ nyumbani kwangu hawajakuta chochote, hivyo basi nitaendelea kushirikiana na Serikali ili kuhakikisha kuwa washukiwa wa dawa hizo wanafikishwa kwenye mikono ya sheria,” alisema Gwajima.
Askofu Gwajima aahidi kutoa ushirikiano Polisi Askofu Gwajima aahidi kutoa ushirikiano Polisi Reviewed by Zero Degree on 2/14/2017 11:27:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.