Clattenburg ameachana na ligi Kuu ya Uingereza na kujiunga na shirikisho la soka la Saudi Arabia
Mwamuzi mkongwe katika soka la nchini Uingereza Mark Clattenburg anaondoka rasmi kunako ligi ya nchi hiyo na anaelekea nchini Saudi Arabia kulitumikia shirikisho la soka la nchi hiyo.
Clattenburg mwenye umri wa miaka 41, ambaye alifanya vizuri mwaka jana akichezesha Fainali kubwa tatu ikiwemo ile ya EURO nchini Ufaransa, fainali ya FA cup pamoja na Fainali ya Klabu bingwa Ulaya, anaelekea Saudi Arabia kuwa mkuu wa kitengo cha waamuzi wa nchi hiyo, taarifa iliyothibitishwa na Bodi ya Waamuzi wa Ligi kuu ya Uingereza.
Tayari amekwisha pangiwa majukumu yake mapya ambayo ni kuhakikisha timu za nchi hiyo zinafanya vizuri na kufanya ligi ya Saudi inakuwa ya kitaalamu zaidi , hata hivyo anatarajiwa pia kuwa msiamamizi mkuu wa baadhi ya michezo ya ligi kuu nchini humo.
Mchezo wake wa mwisho kuchezesha katika ligi kuu ya Uingereza ni mchezo wa wiki iliyopita ambao Arsenal alishinda goli 2-0 dhidi ya Hull City.
Tayari amekwisha pangiwa majukumu yake mapya ambayo ni kuhakikisha timu za nchi hiyo zinafanya vizuri na kufanya ligi ya Saudi inakuwa ya kitaalamu zaidi , hata hivyo anatarajiwa pia kuwa msiamamizi mkuu wa baadhi ya michezo ya ligi kuu nchini humo.
Mchezo wake wa mwisho kuchezesha katika ligi kuu ya Uingereza ni mchezo wa wiki iliyopita ambao Arsenal alishinda goli 2-0 dhidi ya Hull City.
Clattenburg ameachana na ligi Kuu ya Uingereza na kujiunga na shirikisho la soka la Saudi Arabia
Reviewed by Zero Degree
on
2/17/2017 01:16:00 PM
Rating: