Loading...

David Beckham afunguka kuhusu klabu yake ya zamani, Manchester United.

Winga wa zamani wa Manchester United, David Beckham amesema hakuiitazama timu hiyo kwa miaka mitatu Old Trafford tangu alipojiunga na Real Madrid.

Baada ya kunyakua mataji sita ya Ligi Kuu England na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Beckham aliondoka katika klabu hiyo iliyomkuza na kujiunga na kwa uhamisho ghali wa wakati huo wa Euro 35 milioni kujiunga na Madrid 2003.

Uhusiano wa Beckham na kocha Alex Ferguson ulifikia mwisho, kitu kilichomfanya raia huyo wa Scotland kuidhinisha Beckham kujuiunga na Real, ingawa awali angeweza kujiunga na Barcelona.

Hata hivyo, Beckham, ambaye alishika nafasi ya pili katika tuzo za mwanasoka bora wa Dunia 1999, alisisitiza kuwa hakuitazama Manchester, klabu ambayo alianza kuitumikia akiwa mtoto 1991.

“Sikuitazama Manchester United miaka mitatu (baada ya kuondoka),” alisema nyota huyo wa zamani alipozungumza na BBC Radio 4’s Desert Island Discs.

Beckham aliongeza: “Nilipatwa na mshtuko na kuchanganyikiwa kwa sababu ndiyo kwanza tulikuwa tumetwaa ubingwa wa Ligi Kuu mwaka ule.

“Bila ubishi nilitaka kucheza hadi kuzeekea Old Trafford, kwa sababu Manchester United ilikuwa timu yangu. Sikuwa na wazo la kuondoka Manchester United kabisa.
David Beckham afunguka kuhusu klabu yake ya zamani, Manchester United. David Beckham afunguka kuhusu klabu yake ya zamani, Manchester United. Reviewed by Zero Degree on 2/01/2017 01:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.