Loading...

Gari la shule laua watu wanne mkoani Kagera

Watu wanne wakiwemo waendesha bodaboda wawili na wafanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la soko la Rwamishenye lililoko katika Manispaa ya Bukoba wamepoteza maisha baada ya kuparamiwa na gari la shule ya Mbunge wa jimbo la bukoba vijijini Jasson rweikiza lenye usajili T.377 BZW lililoacha njia wakati likiwarudisha majumbani mwao wanafunzi wa kutwa wanaosoma shule hiyo.

Akizungumzia juu ya tukio hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani kagera, kamishina msaidizi mwandamizi, augustine Ullomi amesema ajali hiyo imetokea katika eneo la Rwamishenye baada ya gari hilo lililokuwa linaendeshwa na Josiah Kasingwa anayeshikiliwa kwa uchunguzi zaidi.


Amewataja waendesha pikipiki waliopoteza maisha kuwa pamoja na Damian Augustino na mtu aliyemtaja kwa jina moja la Denis na wafanyabiashara katika soko la Rwamishenye amewataja kuwa ni Patricia Patric na Frolence Innocent.

Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara katika soko kuu la Rwamishenye walioshuhudia tukio akiwemo mama mmoja aliyekuwa na mtu mmoja ambaye ni miongoni mwa watu wanne waliopoteza maisha wanaeleza hali ilivyokuwa na hatua walizozichukua katika kuokoa maisha yao wakati wa tukio hilo.

Source: ITV
Gari la shule laua watu wanne mkoani Kagera Gari la shule laua watu wanne mkoani Kagera Reviewed by Zero Degree on 2/26/2017 11:26:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.