Loading...

Hii hapa ratiba ya 16 bora ya michuano ya kombe la UEFA Europa League

Ratiba ya michuano ya kombe la Uefa Ueropa League katika hatua ya robo fainali imetoka huku michezo ya awali ikitarajiwa kuchezwa Machi 9 na marudiano ikiwa ni Machi 16.

Baada ya kumalizika kwa hatua ya 32 bora ya michuano ya UEFA Europa League, Ijumaa ya February 24 katika mji wa Stockholm Sweden ilichezeshwa droo ya kupanga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo, timu ya KRC Genk inayochezewa na Mbwana Samatta imepangwa kucheza na wapinzania wao KAA Gent.

KRC Genk imepangwa kucheza na KAA Genk zikiwa na timu zote zinazotoka Ubelgiji, hivyo ushindani wa game hiyo hautakuwa wa kawaida, Man United wao wamepangwa na FC Rostov ya Urusi.

Mechi zinazosubiriwa kwa hamu kubwa ni pamoja na Olympique Lyon ya Ufaransa iliyopangiwa kucheza na AS Roma ya Italia na mechi nyingine ikiwa ni Schalke 04 dhidi ya Borussia Monchengladbach (zote zinacheza ligi kuu ya Ujerumani).


Kutokana na kiwango kwa sasa kutoka kwa Manchester United inapewa asilimia kubwa ya kuingia katika hatua ya nusu fainali ya kombe hilo kutokana na kupangiwa timu ya Rostov kutoka Urusi ambayo inashika nafasi ya saba katika ligi ya kwao.

Wakati huo huo timu ya Mbwana Samatta KRC Genk imepangiwa kucheza na KAA Gent (zote kutoka Ubelgiji) ambayo iliitoa Tottenham Hospurs katika hatua ya timu 32 bora.
Hii hapa ratiba ya 16 bora ya michuano ya kombe la UEFA Europa League Hii hapa ratiba ya 16 bora ya michuano ya kombe la UEFA Europa League Reviewed by Zero Degree on 2/25/2017 12:18:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.