Conte naye alikuwa na haya ya kusema kufuatia Leicster City kumtimua Claudio Ranieri
Antonio Conte amekiri kuwa kama meneja ni suala la kusikitisha na kukatisha tamaa kusikia habari ya wachezaji kushiriki katika tukio la kufukuzwa kwa Kocha Claudio Ranieri kutoka Leicester City.
Bosi huyo wa 'The Blues' anasema kwamba ni makosa kwa wachezaji kuamua hatma ya kocha na anakubali kwamba mazingira yatakuwa magumu sana kwa meneja wa soka endapo wachezaji wake watafikia hatua kama hizo.
Conte alisema katika mkutano na waandishi wa habari jana:
"Sipendi kusikia wala kufuatilia aina hii ya habari kwa sababu ni kumkosea heshima Claudio.
"Si haki kwamba wachezaji ndio wanaotakiwa kuamua kwamba meneja afukuzwe au la, kama itatokea hivyo basi hiyo ina maana klabu ni maskini na haina nguvu ya kiutawala.
"Siamini au naweza sema sina imani katika hili.
"Sitaki kusikiliza aina hii ya habari kwani ni kusikitisha kwa meneja.
"Pia kufikiria wachezaji kuwa ndio waamuzi wa nafasi yako ya kazi na nini hatima yako siyo nzuri."
Conte naye alikuwa na haya ya kusema kufuatia Leicster City kumtimua Claudio Ranieri
Reviewed by Zero Degree
on
2/25/2017 12:10:00 PM
Rating: